Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde leo amefanya kikao cha pamoja na wakulima wa zabibu,Uongozi wa UWAZAMAM pamoja na benki ya TADB na kuwaagiza viongozi wa ushirika wa zabibu wa UWAZAMAM kuhakikisha unawalipa wakulima haraka malipo ya zabibu zao walizonunua.
"Haiwezekani wakulima walete zabibu zao kwenu, ambazo mmezichakata na kuwa mvinyo gafi, wamekaa zaidi ya mwezi wakisubiri malipo yao zaidi ya milioni 200, ni lazima viongozi muwajibike kutafuta suluhu ya haraka na kuwalipa wakulima.
Najua UWAZAMAM mmeingia mkataba na wanunuzi wa mchuzi wa zabibu,ambao mkataba huo utumike kama dhamana kupata fedha benki na kuwalipa wakulima.
Serikali inatamani kuuona ushirika huu wa wakulima wa Zabibu unakua na kujenga kiwanda chake wenyewe cha uchakataji wa zabibu,hivyo lazima tuanze sasa kuweka misingi bora na kuwasaidia kufikia malengo yengu” Alisema Mhe. Mavunde.
Aidha,Viongozi wa ushirika huo walimweleza Mhe Mavunde kuwa tatizo Lao ni mtaji, hivyo wamefanya jitihada za kupata mkopo TADB lakini wamekwama kutokana na ukosefu wa hati ya eneo lao ambapo kiwanda chao kipo, hali inayopelekea kuwepo kwa malalamiko hayo ya wakulima kucheleweshewa malipo ya mchuzi wao wa zabibu (mvinyo gafi).
Katika sehemu ya kutatua changamoto hiyo, Mhe Mavunde alimtaka Meneja wa TADB Kanda ya Kati, Ndg. Yodas Mwanakatwe kuangalia uwezekano wa kutumia mkataba wa utatu (Tripartite Agreement) uliopo kati ya wanunuzi, UWAZAMAM na TADB ili waweze kutoa mkopo kwa ushirika huo utakaowezesha ushirika kuwalipa wakulima haraka na kutatua changamoto iliyopo.
Naye Meneja wa Kanda wa TADB, ndugu Mwanakatwe alimweleza Mhe. Mavunde kuwa amepokea maelekezo hayo na kwamba Benki yake wanakwenda kuangalia jinsi ya kutekeleza maagizo hayo, ikiwa ni pamoja a kujadiliana na ushirika namna bora ya kutekeleza mkataba wa utatu (Tripartite Agreement) ili wakulima walipwe haraka iwezekanavyo.
Home
HABARI
KILIMO
NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWATAKA USHIRIKA WA WAKULIMA WA ZABIBU (UWAZAMAM) KULIPA MADENI YA WAKULIMA KWA WAKATI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...