Wananchi wanaohujumu miradi ya maji kuchukuliwa hatua kali za kisheria hasa kwa wale wafugaji wanaoachia Mifugo yao mtaani.

Kauli hiyo ameitoa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe alipotembelea mradi wa maji wa Makongo mpaka Bagamoyo uliogharimu shilingi bilioni 65.

Akizungumza kwenye ziara hiyo Gondwe amesema umefika wakati sasa wa kuwachukulia hatua wafugaji wanaoachia Mifugo yao barabarani na mtaani kwani ndio chanzo kikubwa cha kuharibu miundombinu ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira (DAWASA)

"Nitoe Rai kwa wafugaji wote wa Wilaya ya Kinondoni kuchunga Mifugo yao sehemu ambayo hakuna miundombinu ya maji na ukidhibitika unaharibu miradi ya maji kwa ajili ya Mifugo yako hatutakufumbia macho kwani miradi ya maji yote ni Kodi za wananchi hivyo zinapaswa kusimamiwa vizuri" alisema Gondwe

Pia ametoa pongezi kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira (DAWASA) ikiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja kwa kuweza kusimamia miradi ya maji pamoja na upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kinondoni.

Amesema kuwa ziara yake kwenye mradi hiyo ni kuangalia namna ya kujua palipo na changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo yaliyopo pembezoni wa mji ikiwemo Mabwepande, Mbweni, Bunju, Wazo, Salasala, Goba, Kinzudi, Changanyikeni na Mivumoni na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji na kueleza kuwa amejiridhisha na namna mradi huo unavyoendelea hasa kwa mantenki yanayojengwa.

Naye. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA, Bi Neli Msuya amesema baada ya kumalizika Kwa mradi huo wananchi wa Mabwepande, Mbweni, Bunju, Wazo, Salasala, Goba, Kinzudi, Changanyikeni na Mivumoni wataweza kuondokana na tatizo la maji.

Pia amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe kwa kuweza kutembelea mradi wa maji wa Makongo mpaka Bagamoyo ili kujionea uhalisia wa mradi huo ili akawe balozi mzuri wa DAWASA.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA, Bi Neli Msuya akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe kwenye Tanki la maji la Mabwepande wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Mabwepande, Harouna Taratibu kuhusu ujazi wa Tanki la maji lililopo katika eneo la Mabwepande lenye ujazo wa Lita Milioni 6 wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa DAWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe  akiangalia ujazo wa maji kwenye tenki la Mabwepande wakati wa ziara ya kukagua mradi wa maji wa Makongo mpaka Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akifungulia maji bombani kuhakikisha kama kweli maji yameanza kutoka kwenye mtaa wa Kinondo kata ya Mabwepande wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akizungumza na Mama Mudy wa mtaa wa Kinondo kata ya Mabwepande kuhusu namna anavyopata huduma ya maji wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA katika Wilaya hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akizungumza wandishi wa habari pamoja na wananchi wa mtaa wa Kinondo kata ya Mabwepande wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA
Mwenyekiti wa mtaa wa Kinondo kata ya Mabwepande Mohamed Tajukhan akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mamna walivyoupokea na kusimamia mradi wa maji hasa kuwasambazia wananchi wa mtaa huo maji safi na salama wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe ya kukagua mradi wa maji wa Makongo mpaka Bagamoyo.
Mama Mudy wa mtaa wa Kinondo kata ya Mabwepande akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna alivyofurahia kupata  maji safi na salama kwenye mradi wa maji wa Makongo Hadi Bagamoyo wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa usambazaji maji kutoka makongo Hadi Bagamoyo Mhandisi Grory Reuben kuhusu ujenzi wa tenki la maji la Mbweni litakalokuwa na ujazi wa Lita Milioni 5 wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA
 Meneja wa Mradi wa usambazaji maji kutoka makongo Hadi Bagamoyo Mhandisi Grory Reuben akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe  kuhusu ujenzi wa matenki ya maji kwenye mradi wa maji wa Makongo mpaka Bagamoyo wakati wa ziara ya kukagua mradi huo wa maji
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA, Bi Neli Msuya akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe kuhusu ujenzi wa Tanki la Mbweni wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA
Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Tegeta Victoria Masele akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe kuhusu tenki la Mbweni lenye ujazo wa Lita Milioni 5 litakavyoweza kuwahudumua wananchi wa Mbweni na Bunju wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA
 Ziara ikiendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...