NA FARIDA SAID.MORGORO.
WAANYABIASHARA nchini wametakiwa kuacha kufanya biashara kwa mazoea na badala yake wafuate sharia zilizopo ikiwa ni pamoja na kusajiri jina la biashara au kampuni ili kuondoa usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza kwa baadhi ya wafanyaiashara na wamiliki wa makampuni.

Rai hiyo imetolewa Mkoani Morogoro na Afisa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Bashara na Leseni BRELA Bi. Sweetness Madatu kwenye maonyesho ya tano ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Kwa upande wao wakazi wa Mkoa wa Morogoro waliotembelea banda la BREALA katika viwanja vya Jamhuri wameupongeza Wakala huo kwa elimu wanayoitoa kwa wananchi hao juu ya Umuhimu wa kusajili Bishara zao katika mamlaka hiyo.

Wakizungumza na michuzi Blog wakazi hao wamesema kuwa licha ya kusogezewa huduma kwa ukaribu zaidi hivi sasa wanantambua umuhimu wa kusajili biashara zao kwani itawasaidia kuondosha bughudha katika kuteleza majukumu yao ya kila kisu.

Aidha wamesema kupitia elimu inayotolewa na BRELA inawaongezea uelewa wa kutanua shughuri zao za biashara ndani na nje ya nchini kwani wamekuwa wakitambuliwa kimataifa kupitia majina ya biashara au kampuni zao.

Sanjari na hilo wamesema kuwa usajili wa biashara kwa njia ya mtandao imekuwa huduma rahisi kwani kunamuwezesha mteja kupata cheti chake papo kwa papo hasa kwa wale waishio vijijini na kuondoa usumbufu wa kuzifuata huduma za usajili katika ofisi za BREALA zilizopo Mjini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...