Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe.Thomas Apson Mei 9,2022 ametoa kauli kwa Madereva wote Wilayani Siha kuendesha magari kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka mkono wa
sheria.
Wito huo ametoa katika eneo la Datchi Kona ambapo ajali ya gari kumgonga mtoto wa wa darasa la tatu anayesoma katika shule ya msingi Gararagua.
Mhe Mhe.Thomas Apson ametoa agizo kwa meneja wa TANROAD Mkoa wa Kilimanjaro kufika eneo la tukio tarehe 10 Mei,2022 ili kuona namna ya kuweka matuta katika eneo hilo ambalo ajali za watu kugongwa na magari zimekuwa zikitokea mara kwa mara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...