Familia ya Eng. Lusekelo Ambokile Mwambuli wanasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpendwa Eng. Lusekelo Mwambuli kilichotokea 7/5/2022 katika Taassi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar s Salaam na maziko yatafanyika leo 13/5/2022 nyumbani kwao Mbalizi, Mbeya.

Eng. Mwambuli aliagwa katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kuelekea mkoani Mbeya.

Akitoa salamu katika ibada ya kumuaga Eng. Mwambuli jijini Mwanza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Robert Gabriel alieleza namna marehemu alivyojituma katika kufanya kazi na kushirikiana na jamii kwa moyo wa upendo na ukarimu.

Familia inawashukuru wote kwa ushirikiano na faraja waliyoonesha katika kipindi hiki kigumu wakiwemo madaktari, watumishi wa Mungu, majirani wa Mwanza, Dar es Salaam na Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, wafanyakazi IFM, TRA, COSO Marketing, Tanzania Law Society (TLC,) ndugu, jamaa na marafiki.

Mjane wa marehemu Eng. Lusekelo Mwambuli pamoja na familia wakiaga mwili wa mpendwa wao katika iliyofanyika katika kanisa la KKKT Imani jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Robert Gabriel (wa pili kushoto) akiwa katika ibada ya kumuaga Eng. Lusekeo Mwambuli iliyofanyika katika kanisa la KKKT Imani jijini humo kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...