Mbunge wa Jimbo la Kigamboni  Mh Dkt Faustine Ndungulile leo amezindua kituo cha Huduma kwa wateja cha Kampuni ya TUNZAA Digital Holding yenye makao makuu yake Kigamboni karibu na ofisi za Takukuru mapema leo ijumaa tarehe 08 Julai 2022 akiwa katika kituo hiko amefanikiwa kujionea namna kituo hiko kinavyofanya kazi na ameweza kuona namna wateja wanavyoweza kununua bidhaa kupitia mfumo wa TUNZAA ambao unampa nafasi mteja kulipia kidogo kidogo huku mfanyabiashara akipata taarifa ya manunuzi ya bidhaa yake

Akiwa katika kituo hiko Mh Ndungulile amesema “Nimefurahishwa sana na ubunifu huu na hakika ni sulushisho kwa watanzania ambao wanapenda kununua bidhaa kwa kudunduliza na inampa mteja nafasi ya kutokuwa na deni lakini pia nimefurahishwa na ubunifu kuwa umetoka katika jimbo langu la Kigamboni na pia nawapongeza wamiliki kwa ubunifu huu

Kituo hiki cha huduma kwa wateja kitawasaidia wateja na watanzania kuweza kupata taarifa za namna ya kutumia TUNZAA, kujiunga TUNZAA kama mnunuzi au muuzaji wa bidhaa au Huduma lakini pia kitatoa nafasi kwa watanzania ambao hawana simu janja lakini wangependa kununua kwa kulipa kidogo kidogo ambapo wataweza kutembelea kituo hiko

Mpaka sasa TUNZAA ina watumiaji Zaidi ya 12,000 huku bidhaa zilizolipiwa mpaka sasa kuwa Zaidi ya 7000 huku watumiaji wengine wakiendelea kujiunga na mfumo huu ambao unatoa nafuu kwa wateja kwa kuwapa nafasi ya kulipia bidhaa kidogo kidogo bila kuwa na mawazo wala madeni

Pia TUNZAA inawakaribisha wauzaji wa bidhaa mbalimbali ndani ya Tanzania kuweza kujiunga na TUNZAA kwaajili ya kutanua soko lao kwa watumiaji Zaidi ya 12,000 huku idadi ya watumiaji ikiendelea kukua kwa kasi sana

TUNZAA imekuwa sulushisho la maswala ya kifedha kwa kuwasaidia watanzania kuweza kuweka mipango ya kumiliki au kununua bidhaa zao bila usumbufu wa aina yoyote ule

Ili kuweza kujiunga TUNZAA kama mnunuzi basi uanchotakiwa kufanya ni kupakua mfumo wetu wa TUNZAA kupitia google playstore na Apple store na kujiandikisha, na pia Kama wewe ni mfanyabiashara unaweza kujiunga pia kupitia TUNZAA PLUS inayopatikana katika google store na Apple store

Kwa maelezo Zaidi pia unaweza kutembelea ofisi zetu zilizopo Kigamboni karibu na ofisi za Takukuru au kupiga simu 0673 755217 kwa maelezo zaidi

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Mh Dkt Faustine Ndugulile akisikiliza maelekezo ya namna ya kutumia mfumo wa TUNZAA kutoka kwa Mwanzilishi na mkurugenzi wa TUNZAA Digital mara baada ya kufika katika kituo cha huduma kwa wateja cha TUNZAA kilichopo wilaya ya Kigamboni
Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh Dkt Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya too pamoja na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampuni ya Tunzaa Digital Holding mara baada ya kuzindua kituo cha Huduma kwa wateja cha Tunzaa kilichopo Kigamboni Mlaligi mapema leo Ijumaa tarehe 8 Julai 2022
Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh Dkt Ndugulile ambae alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja cha TUNZAA akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wateja na wafanyakazi wa TUNZAA waliofika katika uzinduzi huo uliofanyika leo Kigamboni .



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...