Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde ameielekeza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kuhakikisha matokeo ya tafiti inazofanya yanawafikia wakulima kwa wakati ili kuongeza tija na kipato chao. 

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 07 Julai, 2022 aliposhiriki Maadhimisho ya Siku ya Kilimo Biashara, Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika viwanja vya Selian vilivyopo Mkoani Arusha.

"TARI mnafanya kazi nzuri, lakini bado mnayo kazi kubwa ya kufikisha utaalamu na teknolojia mnazozigundua kwa wakulima wetu. Wekeni mkazo mkubwa katika kutangaza matokeo na teknolojia hizo ili ziweze kuwa na tija kubwa kwa wakulima.

Watafiti lazima waache utaratibu wa kufungia au kukaa na matokeo ya tafiti na teknolojia maofisini, badala yake kujikita katika ubunifu zaidi wa kufikisha utaalamu huo kwa wakulima. 

Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetupa kipaumbele cha kipekee sisi wakulima, na ndo maana bajeti ya Wizara ya Kilimo imeongezeka kutoka bilioni 294 mwaka 2021/2022 hadi bilioni 954 mwaka 2022/2023.

Bajeti hii iliyoongezeka imeelekezwa katika utekelezaji wa vipaumbele vya kimkakati ikiwemo kuimarisha utafiti, kuongeza uzalishaji wa mbegu bora ili kuongeza mavuno kwa wakulima sambamba na ugunduzi wa mbinu bora za kilimo ili kumsaidia mkulima wa Tanzania kuzalisha kwa tija”Alisema Mavunde

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dkt. Geoffrey Mkamilo alieleza kuwa wamepokea maelekezo hayo ya Mhe. Mavunde na kwamba wameanza utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na kuanzisha maadhimisho ya siku ya kilimo biashara katika vituo vyote vya Kanda vya Utafiti na Viwanja vya Nanenane Nchi nzima, lengo likiwa ni kufikisha matokeo ya tafiti mbalimbali kwa wakulima kwa wakati ili kukidhi malengo tarajiwa ya kumsaidia mkulima wa Tanzania kulima kwa tija.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...