Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

DREVA wa bodaboda Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, Rashid Ally Handiko, amefanikiwa kushinda Sh Milioni 10 za bahati nasibu ya Watanzania Biko kwa kupitia droo yake kubwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki,ikiwa ni mwendelezo wa watu wengi kuendelea kushinda mamilioni ya zawadi kutoka kwenye bahati nasibu hiyo.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Ally alisema amefarijika kuona ameshinda fedha sanjari na kukabidhiwa kwa haraka kiasi cha kuamua kitu cha kuzifanyia kwa ajili ya kuendeleza maisha yake.

"Nashukuru kufanikiwa kushinda fedha zangu na kukabidhiwa bank kwa haraka kwa maana ndio njia ya kuzipatia kazi ya kufanya, ukizingatia kuwa hii njia nzuri ya kukuza uchumi wangu," Alisema Ally.

Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia sh 2500 hadi milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.

Kianzio cha kucheza Biko ni sh 1000 na kuendelea ambapo Watanzania wengi wameendelea kushinda zawadi za papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa za kushinda hadi sh milioni 40, zikiwa na lengo la kuboresha maisha ya wote wanaocheza Biko.

Droo za biko zinafanyika kila Jumapili ambapo Watanzania wengi wamekuwa wakishinda zawadi kubwa za wiki bila kusahau papo kwa hapo zinazoingia moja kwa moja kwenye simu za mkononi.

Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja kushoto akimkabidhi fedha zake Rrashid Ally Sh Milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki. Kulia ni Catherine Momburi Meneja Uhusiano wa bank ya CRDB Tawi Primier Palm Beach, jijini Dar es Salaam


Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, akiwa mwenye furaha kubwa baada ya kufanikiwa kumkabidhi Rashid Ally fedha zake Sh Milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa ya Biko. Picha na Mpiga picha wetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...