Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
TUME ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (Costech) imetakiwa kufanya mapitio ya sheria na sera
zilizopo ili kuhakikisha bunifu zinazozalishwa zinatatua changamoto
zilizopo katika jamii.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia, Juma Kipanga wakati alipotembelea banda la
Costech katika maonesho ya 46 ya Sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es
Salaam.
Amesema wakati sheria hiyo inaanzishwa kulikuwa hakuna
eneo la ubunifu ndani yake ndiyo maana wanataka kufanya mapitio hayo,
kwa sababu wanataka bidhaa zinazobuniwa ziweze kutatua changamoto hapa
nchini.
Amesema wamepiga hatua kama taifa kwa kutengeneza
bidhaa mbalimbali kupitia bunifu za ndani hivyo ni lazima kuhakikisha
bunifu hizo zinawanufaisha kwa kutengeneza ajira.
Hata hivyo,
Kipanga amesema wameona wabunifu mbalimbali walivyoendelezwa na Costech,
kabla ya hapo walikuwa na mfuko wao na pia kuna mashindano yanaitwa
makisatu.
"Vyombo vyote hivi vimeundwa kuhakikisha kwamba
bunifu pamoja na tafiti zinaweza kukuzwa na kuendelezwa ili badae ziwe
bidhaa," amesema Kipanga.
Kipanga ametoa rai kwa Costech
kuendelea kufanya kazi na kushirikiana kwa sababu Taifa hili litajengwa
na watanzania wenyewe na lengo la bunifu hizi ni kuhakikisha zinatatua
changamoto.
"Tutatumia bunifu zetu za ndani kwa sababu ni
rahisi kupata bidhaa inayoweza kutatua changamoto kwa bei rahisi na pia
inaweza kutumika kwa urahisi,"amesema Kipanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...