Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Allan Kijazi akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendelo ya Makazi Dk.Allan Kijazi akipata maelezo wakati akiwa katika banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Sabasaba
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendelo ya Makazi Dk.Allan Kijazi akiwa na wananchi wakiwa na hati ya maeneo ya ardhi walizopata ndani y maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.


Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

 KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Allan Kijazi amesema kuwa Wizara imejipanga katika kuwahudumia wananchi kwenye  upatikanaji wa hati pamoja na upimaji wa maeneo.

Dk.Kijazi aliyasema hayo wakati alipotembelea Maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius J.K Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Wizara inapima mipaka ya Ngorongoro na Loliondo mkoani Arusha  pamoja na kufanya thamini kwa wananchi wanaohama kutoka maeneo kwenda Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga.

Amesema kuwa wananchi watembelee maonesho ya Sabasaba pamoja na kupata huduma mbalimbali kutoka katika kila eneo linalohusiana na makazi.

 
 Dk.Kijazi aidha amebainisha kuwa wanashiriki kila maonesho ili kutanua huduma na kuwahudumia wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...