Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita, Zahra Michuzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tantrade, Latifa Khamis akibadilishana mikataba ya makubaliano kati ya  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrdae) na Halmashauri ya mji wa Geita katika uandaaji wa maonesho ya dhahabu na kuyapandisha hadhi kufikia ya hadi ya itaifa makubaliano hayo yamefanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita, Zahra Michuzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tantrade, Latifa Khamis akisaini mikataba ya makubaliano kati ya  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrdae) na Halmashauri ya mji wa Geita katika uandaaji wa maonesho ya dhahabu na kuyapandisha hadhi kufikia ya hadi ya itaifa makubaliano hayo yamefanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita, Zahra Michuzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tantrade, Latifa Khamis wakionesha mikataba ya makubaliano kati ya  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrdae) na Halmashauri ya mji wa Geita katika uandaaji wa maonesho ya dhahabu na kuyapandisha hadhi kufikia ya hadi ya itaifa makubaliano hayo yamefanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tantrade, Latifa Khamis akizungumza mara baada ya kusaini mikataba ya makubaliano kati ya  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrdae) na Halmashauri ya mji wa Geita katika uandaaji wa maonesho ya dhahabu na kuyapandisha hadhi kufikia ya hadi ya itaifa makubaliano hayo yamefanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.


SERIKALI kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrdae) na Halmashauri ya mji wa Geita wameingia makubaliano ya ushirikiano kwa kutiliana saini katika uandaaji wa maonesho ya dhahabu na kuyapandisha hadhi kufikia ya hadi ya itaifa.

Maonyesho hayo ya dhahabu ambayo yanayotarajiwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu hapo awali yalikuwa yakifanyika ki mkoa na sasa yatafanyika kitaifa

Makubaliano hayo yameingiwa leo Juni 4, 2022 jijinj Dar es Salaam Salaam wakati wa maonyesho ya 46 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule amesema makubaliano hayo yatakwenda kuyafanya maonesho hayo ya dhahabu kuwa makubwa kuliko yote yanayofanyika hapa nchini.

Amesema maonesho hayo ya dhahabu kuwa ya kitaifa yatasaidia kukua na kuwavutia wawekezaji wengi ndani na nje ya nchi kushiriki katika kuonesha bidhaa zao.

"Tunafahamu kuwa muda uliobakia ni mchache kwani Septemba ndiyo yatafanyika maonesho ya dhahabu mkoani Geita, tumeshawaambia wadau kuwa hatutayapeleka mbele hivyo kwa kushirikiana na Tantrade tutakaa pamoja na kukubaliana namna bora ya kuyaboresha ili yaonekane ya hadhi na kisasa," amesema

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita, Zahra Michuzi amesema makubaliano hayo yatasaidia kuleta mapinduzi na kufanya mabadiliko kwenye teknolojia ya dhahabu ndani ya mkoa wa Geita.

Amesema wanataka kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya madini ya dhahabu hivyo kupanda hadhi kwa maonesho hayo kutachagiza mabadiliko hayo

"Tumepokea kwa furaha nia njema ya kuingia makubaliano na Tantrade kwani kutafanga maonesho hayo kutambulika nchini na kupanua wigo mpana wa ufanyaji biashara," amesema

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tantrade, Latifa Khamis amesema kusainiwa kwa makubaliano hayo kutakwenda kuimarisha na kuufanya uwanja wa Geita kuwa wa kisasa kwa ajili ya maonesho ya dhahabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...