Wakati huu Kampuni imeamua kuwatumia watu maarufu na wahamasishaji
kuichangia Jamii, ambapo mashuti ya penati yanatoa thamani ya mchango ambao mtu
huyu anayepiga anaisaidia Meridianbet
kuichangia Jamii. Kila shuti linalofikia nyavu limepewa thamani ya TSH 50,000.
Baada ya kushinda mashuti kadhaa kati ya mikwaju mitano anayotakiwa kupiga,
mhamasishaji anachagua kundi gani la jamii lisaidiwe kwa fedha hizo.
Wakiwa na balozi wao, na mhamasishaji Jemedari Saidi
Kazumari aliyepiga penati 5 na kupata 4 kati ya hizo na kufanikiwa kukusanya
kiasi cha shilingi laki 200,000/=. Jemedari alipendekeza fedha hizi zipelekwe
kwenye taasisi ya tiba ya CCBRT.
Meridianbet
iliwasilisha fedha hizo CCBRT, ambao walitoa utaratibu sahihi wa kupekela kiasi
kile kwa walengwa ambao ni watu wanaohitaji huduma za kitabibu hospitalini hapo.
Uongozi wa CCBRT ulielekeza kiasi hicho kwenye matibabu ya
mtoto Agness Elias aliyepaswa kufanyiwa upasuaji wa miguu ambao gharama za
upasuaji na matibabu ya kiasi cha 250,000/=.
Viongozi kutoka Meridianbet
waliongeza fedha zaidi ili kukidhi gharama za matibabu, kiasi cha shilingi elfu
50,000/= kikiongezwa kwenye shilingi 200,000/= iliyopatikana awali kwa mikwaju
ya penati nne alizoshinda jemedari, kukamilisha shilingi 250,000/= kwa ajili ya
matibabu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...