Na Mwamvua Mwinyi, KIBAHA


KIASI Cha sh.Milioni 68 za Mfuko wa Jimbo Kibaha Vijijini, Mkoani Pwani zilizotolewa kwenye vipindi viwili zimewezesha kuanzisha ujenzi wa shule tatu za Sekondari jimboni hapo, ili kuinua na kuboresha sekta ya elimu.

"Milioni 34 za kwanza nilianzisha shule ya Sekondari Disunyara, Serikali ikaongeza madarasa sasa yapo zaidi ya kumi, pia nikaanzisha shule mbili mpya za Kawawa nayo imepokea wanafunzi, hivi sasa sekondari ya tatu imeshaanza kujengwa Boko,"

Mafanikio hayo yalisemwa na Mbunge wa Jimbo hilo , Michael Mwakamo, wakati wa ziara yake ya kuzungumza na baadhi ya Wakazi wa vitongoji ,Jimbo la Kibaha Vijijini.

Mwakamo Alifafanua, Matumizi mazuri ya fedha za Mfuko wa Jimbo wa sh. milioni 68 kwa vipindi viwili, yamembeba ambapo kwasasa ameongezewa sh.milioni 20.

Alieleza ,kuongezwa kwa kiasi hicho cha fedha sasa kinaliwezesha jimbo kupokea sh.milioni 54 kwa mwaka, kutoka milioni 34 zilizokuwa zinapokelewa kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi.

"Nikiwa bungeni niliomba Serikali iniongezee fedha za mfuko wa Jimbo, lakini niliambiwa jimboni kuna watu 70,000 hivyo milioni 34 zinanitosha,nikawaomba watembelee miradi niliyoitekeleza katika kipindi changu cha ubunge ,wakajionea namna nilivyozitendea haki fedha zile na Sasa nashukuru ,fedha zimeongezwa naamini tutafanya makubwa ".

Alieleza, baada ya Serikali kutuma watu wake jimboni na kujionea ,waliridhishwa na matumizi ya mfuko huo na Sasa tumeongezwa kiasi cha shilingi milioni 20, hivyo mfuko huo utakuwa unapokea sh. milioni 54 kila mwaka.

"Pamoja na mafanikio yote ambayo sijayazungumza yote , niwaombe wananchi wenzangu tujiandae kikamilifu kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi, linalotarajia kufanyika agost 23 mwaka huu, sensa imeandaliwa na Serikali yetu chini ya Rais Samia Suluhu inalengo la kutambua watu wake ili ipange vizuri mipango yake,"Twende tukajitokeze kutimiza azma hii, alihimiza Mwakamo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...