Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana vipaumbele vya Wizara hiyo kwa mwaka fedha 2022/2023 jijini Dar es Salaam.

*Aipongeza kwa kazi wanazozofanya katika kutunza kumbukumbu za watanzania

Na Chalila Kibuda, Michuzi Blog.
 
WAIRI wa Katiba na Sheria Dkt.Damas Ndumbaro amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa bajeti hii ni kuiwekea nguvu Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ili kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi

Dkt.Ndumbaro ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam amesema kuwa RITA ni chommbo mhimu katika kutunza kumbukumbu ya matukio mbalimbali.

Amesema kuwa amesema kuwa RITA inatakiwa kwenda kidjijitali kwa kuunganisha vyombo mbalimbali vya kutoa haki ikiwemo Mahakama na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Amesema kuwa RITA inafanya kazi kubwa sana ambapo wanatakiwa kupongezwa hivyo kwa mwaka huu tunakwenda kuiongezea nguvu zaidi.

"RITA wanafanya kazi kubwa kwa kutunza takwimu za matukio sasa tutakwenda kidijitali kwa kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi kwa upande wa mahakama." Amesema Dkt.Ndumbaro.

Aidha amesema kuwa kazi ya kusajili inaendelea kwa wanafunzi wa shule ya msingi ambapo baadae kutakuwa hakuna mtu ambaye hana cheti za kuzaliwa.

Dk.Ndumbaro amesema kuwa kasi ya RITA wakiongezewa nguvu watakuwa na uwezo mkubwa katika kutunza takwimu na matukio ya watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...