Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

MKUU wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ,amepokea Pembejeo (Viuatilifu) kwa ajili ya zao la Korosho, katika ghala la CORECU, wakati akiwa kwenye ziara Wilayani Kibiti.

Akipokea Viuatilifu hivyo Mkuu huyo wa mkoa amesema ,mkoa huo uliomba Viuatilifu Tani 1,600 za Salfa ya unga ambapo hadi sasa umepokea Tani 804 .

Aidha Kunenge ameeleza,viuatilifu vya maji Mkoa uliomba Lita 100,000 hadi sasa wamepokea lita 109,000 na lita zingine elfu 15 zitaletwa.

Pamoja na hilo,ameeleza kuwa Mkoa msimu wa mwaka 2020 ulipata Tani 7000, mwaka 2021 Tani 11,000 na mwaka huu wanatarajia kupatiwa Tani 15,000 hadi 20,000.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...