Na. MatukioDaimaAPP,  Songwe

KAMANDA wa Kikosi Cha usalama barabarani Tanzania Wilbroad Mutafungwa ameongoza oparesheni ya ukaguzi wa Malori ya mizigo yanayoingia nchini kutoka nchi za kusini mwa Tanzania na kukamata Malori mabovu 119 huku matano yakisafirisha kontena za mizigo pasipo kufunga loock zake .

Oparesheni hii rafiki Kwa madereva imelenga kufanya matengenezo ya Malori ya mizigo yanayoingia nchini Tanzania kutokea nchi za kusini mwa Tanzania ili kuepusha ajali nchini .

Akizungumza na madereva eneo hilo la Oparesheni Mutafungwa amewataka madereva hao kutoa ushirikiano Kwa askari wa usalama barabarani na kuwa zoezi la ukaguzi litakuwa ni endelevu na litafanyika mkoa wa Songwe,Mbeya ,Makambako mkoani Njombe pamoja na Pwani japo mikoa mingine pia itakuwa na ukaguzi pale inapobidi kufanya hivyo .

Mutafungwa alisema kupitia oparesheni hiyo ya ukaguzi wa Malori jumla ya Malori 422 kati ya Malori hayo 119 yalikutwa na ubovu na Malori matano hayakuwa na loock kwenye makontena yaliyokuwa yamebeba jambo ambalo ni hatari kubwa.

Hata hivyo alisema baada ya kufanya ukaguzi huo Kuna tabia ambazo wamezibaini zinazofanywa na baadhi ya madereva za kuregeza Breck ili kuongeza spidi kwenye Malori hayo na kuwa wakati mwingine hatua Kali Kwa madereva wanaofanya hivyo zitachukuliwa .

Aidha Kamanda Mutafungwa alisema oparesheni kama hiyo imefanyika kwenye Mabasi ya Abiria na vyombo vingine na kuwa Kwa Sasa atakutana na wamiliki wote wa Malori nchini ili kuzungumza nao na kuwa na mkakati wa pamoja wa kuthibiti ajali zinazosababishwa na ubovu wa Malori.

Kupitia oparesheni hii askari wa usalama barabarani baada ya kufanya ukaguzi na kubaini ubovu wa Lori ,wamekuwa wakitoa plat namba na kisha kumpigia simu mmiliki wa Lori husika ili Lori Hilo litengenezwe kabla ya kuendelea na safari hatua ambayo madereva wamepongeza Kwa madai inasaidia.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...