
Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe.Dkt Selemani Jafo akizungumza na wataalam wa Baraza la hifadhi la mazingira NEMC, katika maonesho wakati wa mkutano wa AMECEA ..jpeg)
.jpeg)
PONGEZI zimetolewa na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe.Selemani Jafo alipokuwa akiongea na waandishi wahabari mara baada ya Mkutano wa 20 wa (AMACEA) wenye lengo la kujadili athari za maendeleo katika mazingira uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Amesema NEMC kama taasisi inayoshughulika na masuala ya mazingira imefanya jitihada za dhati katika kuhakikisha sheria ya mazingira ya Mwaka 2004 inatekelezwa kwa vitendo.
"Niishukuru sana Taasisi yetu ya NEMC ambayo kwa sasa hivi Ile enforcement yetu ya sheria wamekuwa wakiifanyia kazi kubwa sana" Amesema Jafo.
Aidha amezitaka taasisi binafsi kushirikiana na wadau wa mazingira pamoja na Serikali katika kuhakikisha wanatunza na kuyahifadhi mazingira kwani hali iliyopo sasa imeambatana na changamoto kubwa za ongezeko la mabadiliko ya hali ya hewa, ukame na kuongezeka kwa kiwango cha maji ya bahari.
"Niwaombe sana wadau mbalimbali tuhakikishe tunashirikiana na taasisi zetu zilizopewa jukumu la kutunza mazingira watambue ya kwamba wanapotimiza wajibu wao wajue kwamba wanafanya kwa niaba ya Nchi yetu ili iweze kuwa salama wakati wote" Amesisitiza Jafo.
Pia amewataka watanzania wote kutambua ya kwamba suala la mazingira ni mtambuka na endelevu hivyo yapasa kila mmoja kuwajibika katika nafasi yake kwa maslahi mapana ya Taifa na kwa maendeleo endelevu ya dunia.
Katika hatua nyingine Mhe.Jafo amewataka wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanatekeleza agizo la Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania la kuandaa mpango mkakati wa usafi wa kila wiki katika maeneo yao ili kutunza na kuhifadhi mazingira.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...