Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dk.Stephan Ngailo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali mbolea nchini na mikakati ya Serikali , jijini Dar es Salaam.

*Ni kutoa mbolea ya ruzuku kwa bei wakulima kumudu

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SERIKALI kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imewahakikishia wananchi katika msimu wa kilimo watambata mbolea kwa bei ya ruzuku kutokana na gharama za mbolea kupanda kwa asilimia 100.

Kupanda kwa kwa mbolea huko kunatokana na athari za Uvico-19 pamoja na vita ya Urusi na Ukraine ambapo soko la mbolea dunani imepanda na Rais Samia Hassan Suluhu ametoa ruzuku ya sh.bilioni 150.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt. Stephan Ngailo amesema kuwa wakulima watapata mbolea kupitia mawakala katika maeneo yao.

Dkt.Ngailo amesema kuwa wakulima nchi nzima wanatakiwa kujisajili kwenye maeneo yao wakati ukifika wa msimu wa kulima watapata mbolea yenye ruzuku ya serikali na hakutakuwa na udanganyifu wa mfumo huo.

Dkt.Ngailo amesema kuwa mbolea zimepanda kwa wastani wa bei ya kufikishia mbolea ya DAP hapa nchini (CIF) kwa mwezi Juni ilikuwa dola za Kimarekani 410 kwa Tani ikilinganishwa na wastani wa dola za Kimarekani 857 kwa mbolea iliyoingia mwezi Juni 2022 sawa na ongezeko la asilimia 109.

Dkt.Ngailo amesema mbolea ya DAP imepanda kutoka sh.55, 843 mwezi Juni 2020 hadi kufikia sh.126, 607 kwa mwezi Juni 2022 kwa mfuko wa kilo 50 na mbolea ya Urea imepanda kutoka sh.52, 500 mwezi Juni 2020 hadi kufikia sh.129, 512 kwa mwezi Juni 2022 kwa mfuko wa kilo 50 katika ongezeko hilo sawa na asilimia 127 na asilimia 147 mtawalia.

Dkt.amesema kuwa ruzuku ya mbolea kwa wakulima utazingatia mahitaji halisi kulingana na taarifa za usajilo na bajeti ya serikali iliyotengwa .

Aidha amesema mbolea ya ruzuku ni mbolea ya kupandia na kukuzia DAP na Urea kwa ajili ya kukuzia Urea mbazo ni takribani ya asilimia 50 ya matumizo ya mbolea nchini huku mbolea za kupandia na kukuzia za aina zingine zitahusiishwa katika mfumo kutokana na soko.

Hata hivyo amesema mfumo wa huo wa mbolea ya ruzuku ni wa kidijitali katika uratibu kutengeneza mnyororo wa wakulima kunufaika na mbolea kutokana na Rais Samia Suluhu kuhakikisha wakulima wanapata mazao na kufanya nchi kuwa na chakula cha kutosha.

Dkt.Ngailo amesema kampuni zitazoingiza na kuzalisha mbolea nchini na kufungasha katika mifuko ya kilogram 25 na 50 ambayo itaandikwa Mbolea ya Ruzuku na itachapwa alama maalum ya mfumo wa kidijitali itakayotolewa TFRA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...