
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dkt. Rashidi Chuachua (wa pili kshoto) akikata utepe ishara ya uzinduzi wa duka linalotembea ‘Vodacom Mobile Shop’ la kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja wao katika maeneo ambayo hayana maduka katika kanda ya nyanda za juu kusini na hasa vijijini. Kushoto ni George Lugata Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji Vodacom Tanzania Plc.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dkt. Rashidi Chuachua na Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji Vodacom Tanzania Plc, George Lugata wakiteta jambo ndani ya duka linalotembea “Vodacom Mobile shop” mara baada ya uzinduzi wa duka hilo uliofanyika Kabwe, jijini Mbeya jana. Vodacom imedhamiria kufikisha huduma kwa wateja wake katika maeneo ambayo hayana maduka kwa kanda ya nyanda za juu kusini na hasa vijijini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...