
WAJUMBE wa bodi ya makamishina ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) tarehe 5 Julai, 2022 watembelea miradi ya Utafiti na Ubunifu visiwani Zanzibar.
Miradi hiyo ni ya utengenezaji wa nyenzo inayotokana na maganda ya miwa kwaajili ya kusafishia majitaka yanayotoka hospitalini pamoja na mradi wa kuongeza thamani ya dawa za asili na kuhifadhi mimea tiba inayotumika kutibu magonjwa yasioambukiza Zanzibar.
Miradi hiyo imefadhiliwa na COSTECH kupitia mfuko wake wa kuendeleza Sayansi Teknolojia na Ubunifu MTUSATE
Aidha COSTECH kupitia MTUSATE imewekeza kiasi cha shilingi milioni100 katika Taasisi ya Utafiti wa Afya na tiba (ZAHRI) ili kugharamia utekelezaji wa miradi hiyo.
Pia wajumbe hao walitembelea maabara za mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar na kupata maelezo mafupi kuhusu miradi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...