SERIKALI kupitia Mradi wa Kuzuia Sumu Kuvu wa 'Tanzania initiative for preventing aflatoxin contamination' (TANIPAC) katika Wizara ya Kilimo imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 80 kwa ajili ya kutekeleza Kudhibiti Sumu kuvu nchini ambapo una lengo la kuelimisha jamii kuhusiana na athari za sumu na udhibiti wake.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maonesho ya kimataifa ya biashara ya 46, Mtaalamu wa Sayansi ya chakula kutoka Idara ya Usalama wa Chakula, Wizara ya Kilimo, Mercy Butta amesema mradi huo ulianza 2019 na unatarajiwa kumalizika 2024 na umekuwa msaada mkubwa kwa jamii hasa wakulima na Wafugaji.
Tanzania mradi huo upo katika Halmashauri 18 ambazo ni Halmashauri ya Itirima, Buchosa, Bukombe, Kasulu, Kibondo, Urambo, Wilaya ya Nzega, Bahi, Kongwa, Chamba, Babati, Kiteto, Kilosa, Gairo, Nanyumbu, Namtumbo na Newara kwa upande wa Zanzibar ni Unguja na pemba.
“Tulianza mradi huu mwaka 2019 tangu tumeanza mpaka sasa tumeweza kuwafundisha wakulima 61,410 kuhusiana na udhibiti wa ubora wa mazao baada ya mavuno, lengo lilikuwa tuwafikie 60,000, ila tumepitiliza lengo hilo, sasa hivi tunajipanga kwenda tena kuwapa elimu ya kabla ya kuvuna, tunaamini wakiwa na uelewa wa kutosha tunaweza kulidhibiti tatizo hili.” amesema Mercy
Pia walipanga kutoa mafunzo kwa maafisa ugani 669 mpaka sasa mwameshatoa mafunzo kwa maafisa 1351 kwa Tanzania nzima, akizungumzia idadi kuwa kubwa Merce amasema kuwa walikuwa na lengo la kutoa mafunzo kwa wakulima pekee ila idadi imeongezeka kwasababu sumu Kuvu inapita mpaka kwenye mifugo.
Hata hivyo amesema sumu kuvu ni hatari kwani ikiingia kwenye mazao ni vigumu kutoka iwe kwa kupika au kukaanga hivyo wataendelea kutoa elimu kupitia mradi huo ili kuweza kumaliza tatizo hilo hapa nchini.
“Mradi huu ulikuja baada ya mwaka 2016 kuwepo kwa watu walithibitika kwamba walipoteza maisha kwa sababu ya kula chakula kilichokuwa kimechafuliwa kwa kiwango kikubwa na sumukuvu, wengine waliugua kwa muda mrefu, kutokana na tatizo hilo serikali iliamua kuja na mradi huu.” Amesema Mercy
Amefafanua kuwa ili kuweza kudhibiti sumukuvu wakulima wanapaswa kufuata kanuni bora za kilimo ikiwemo kupanda kwa nafasi pamoja na kuvuna kwa wakati.
Amesema haiku kwaajili ya kuelimisha jamii peke yake ipo katika Ujenzi wa miundombinu itakayosaidia kuhakikisha suala la sumu Kuvu linadhibitiwa.
Katika kuwaelimisha wananchi teyari wameshawajengea Uwezo Maafisa Ugani, Viongozi ngazi ya taifa hadi wilaya, Wandishi wa habari, wasafirishaji, Wasindikaji wa bidhaa mbalimbali hususani wa Mahindi na Karanga.
Mtaalamu wa Sayansi ya Chakula Katika Idara ya Usalama wa Chakula Kutoka Wizara ya Kilimo, Mercy Butta akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere maarufu sabasaba jijini Dar es Salaam.
MtaalamuUsalama wa Chakula, Hilda Shegembe akizungumza na wananchi wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere maarufu sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Usalama wa Chakula, Kutoka Wizara ya Kilimo, Hilda Shegembe akiwa na Pendo Nsanya Wakionesha moja ya mbinu ya Kukomesha Sumu Kuvu Shambani wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere maarufu sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Usalama wa Chakula, Kutoka Wizara ya Kilimo, Hilda Shegembe akiwa na Pendo Nsanya Wakionesha moja ya mbinu ya Kukomesha Sumu Kuvu Shambani wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya J.K.Nyerere maarufu sabasaba jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...