Na Karama Kenyunko Michuzi TV
KAMPUNI ya simu ya mkononi Vodacom, imezindua kampeni inayoitwa ‘M-Pesa imeitika', Ikiwa na lengo kuhimiza matumizi ya kidijitali ya M-pesa kwenye shughuli za bima, afya, mikopo, kutuma na kupokea pesa nje ya nchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Julai 6, 2022 Mkoani Dar es Salaam, Mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara na masoko wa Vodacom, Tulisindo Mlupilo amesema, katika kampeni hiyo watabadirisha maisha ya wananchi wengi kwa kutumia Teknolojia na kuiongoza Tanzania kuelekea katika zama za kidijitali.
“Tuna mtazamo wa kuiongoza Tanzania kuelekea katika zama za kidijitali na kubadilisha maisha kwa kutumia teknolojia kupitia uchumi wa kidijitali pamoja na ushushwaji wa tozo ili kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma za kidijitali.” amesema Mlupilo.
Ameongeza kuwa, katika kampeni hiyo itakayodumu kwa wiki nane Vodacom itakuwa ikitoa zawadi za kila siku, kila wiki, pamoja na zawadi nono itakayotolewa kwa wale wateja ambao watachukua fursa ya tozo mpya ya huduma iliyopunguzwa kwa kutumia huduma za M-Pesa pamoja na kutumia huduma zingine za M-Pesa kama Vodabima, M-Pesa Visa card na mengine mengi.
Amezitaja zawadi hizo kuwa ni pamoja na bajaji, bodaboda, kujaziwa mafuta ya gari, miezi mitatu ya bima ya ajali, na mwisho wa kampeni kutakuwa na zawadi kuu ambayo ni nyumba mpya iliyojengwa jijini Dar es Salaam yenye thamani ya Shilingi milioni 100.
Amesema, tangu kuanzishwa kwa mfumo wa M-PESA, Vodacom Tanzania mwaka 2008, wamekuwa wakiongeza ubunifu wenye tija kwani mpaka sasa, mfumo umeongoza kwa kutoa huduma za kutuma na kupokea pesa kutokana na urahisi wa matumizi pamoja na usalama wake.
M-PESA imekuwa maarufu kwa matumizi na mahitaji ya malipo ya kibiashara. Vodacom imejitahidi kuongeza huduma mpya zinazopatikana kupitia mfumo wa M-PESA na sasa watumiaji wanaweza kupata mikopo midogo midogo kupitia SONGESHA na M-PAWA. Vikundi vya kijamii vinatumia huduma ya M-KOBA kutimiza malengo yao.
Kampeni hiyo imezinduliwa na moja ya vivutio vya kampeni, ‘wese’, kupitia shindano la ‘wese’, madereva watakaonunua aina yoyote ya bima kupitia huduma ya VodaBIMA watapata nafasi ya kushinda mafuta ya petrol au dizeli yenye thamani ya Shlingi 20,000 kwenye vituo vinavyoshiriki na vile vile washindi 10 watabahatika kujaziwa tenki.
Ili kushiriki, watumiaji wanahitaji kufanya muamala wowote kupitia M-Pesa, kuanzia kutuma pesa hadi kufanya malipo ya serikali au kulipia huduma kama za VodaBIMA. Piga Namba *150*00#, kisha chagua muamala wowote wa M-Pesa
Mkuu wa Idara, maendeleo ya biashara M-Pesa, Tulisindo Mlupilo akimuwekea mafuta dereva wa bodaboda, Alli Juma eneo la Manzese leo Julai 6, 2022, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya M-Pesa Imeitika ikihusisha huduma ya Wese activation ambapo madereva 125 wa boda boda walipata offer ya kuwekewa mafuta bure wanapolipa kwa M-Pesa Kampeni hii Itawazawadia wateja wa M-Pesa kila wanapotumia huduma za kidigitali za M-Pesa. Wengine wapili kulia ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Hatari na Utii wa sheria Vodacom Tanzania Plc, Agapinus Tax na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Digitali na huduma za ziada wa kampuni hiyo Nguvu Kamando.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...