WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amekutana na Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini, Mhe. Matsie Angelina Motshekga ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.

Wakati wa kikao chao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam leo tarehe 5 Julai 2022, Mawaziri hao walijadili pamoja na mambo mengine, namna nchi zao zitakavyoweza kushirikiana katika sekta ya elimu.

Mhe. Motshekga anayetarajiwa kusaini Hati ya Makubaliano na Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda kuhusu Tanzania kushirikiana na Afrika Kusini kufundisha Kiswahili katika nchi hiyo, alisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuainisha maeneo ya kipaumbele ya aina ya elimu tunayoihitaji ili tuweze kubadilishana uzoefu katika maeneo hayo.

Maeneo mengine ambayo viongozi hao waliyadili ni pamoja na programu za kubadilishana wanafunzi na walimu na changamoto zinazoikabili sekta za elimu za nchi hizo ambazo ni pamoja na uhaba wa miundombinu, mimba za mapema, kuacha shule na uhaba wa vitabu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberrata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini Mhe. Matsie Angelina jijini Dar Es Salaam.
Ujumbe ulioambatana na Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini Mhe. Matsie Angelina ukifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberrata Mulamula na Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini Mhe. Matsie Angelina jijini Dar Es Salaam.




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberrata Mulamula na Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini Mhe. Matsie Angelina wakiendelea kujadili masuala ya elimu kuhusu nchi zao huku ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa makini.




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberrata Mulamula akiwa na mgeni wake, Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini Mhe. Matsie Angelina baada ya mazungumzo yao.




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberrata Mulamula na Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini, Mhe. Matsie Angelina wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe walioambatana nao kwenye mazungumzo yao yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...