Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angelina Mabula akimsikiliza Meneja Uhusiano na mawasiliano, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Pendo Gondwe wakati alipotembelea banda la TIC katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashra yanayofanyika katika Viwanja vya JK.Nyerere maarufu kama sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano na mawasiliano, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Pendo Gondwe akizungumza na wananch waliotembelea banda la banda la TIC katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashra yanayofanyika katika Viwanja vya JK.Nyerere maarufu kama sabasaba jijini Dar es Salaam.

Ikiwa Tanzania ina Hekari zaidi ya Milioni 44 kwaajili ya Uwekezaji hivyo wawezaji wameaswa kuja kuwekeza nchini kwani kuna ardhi ya kutosha na asilimia 20 ya ardhi hiyo imeweza kutumika katika kilimo cha Biashara.

Ikiwa Zaidi ya Tanzania 200 wametembelea banda la TIC siku ya Julai 7, 2022 Katika maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya 46 yanayofanyika katika Viwanja vya JK.Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar Es Salaam

Amesema kuwa waliotembelea katika maonesho hayo wengine ni wawekezaji wenye nia ya kuwekeza wengine wameshapelekeza barua kwaajili kupata vibali ya kuwekeza nchini.

Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano na mawasiliano, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Pendo Gondwe pia amewahamasisha watanzania na wawekezaji kuwekeza kwenye Kilimo.

Amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani amekuwa Mstari wa mbele kutangaza Utalii na TIC imeona ni wakati Mwafaka wa kuhakikisha kuwa wanatekeleza juhudi zilizofanywa na Rais.

"Sisi kama TIC tunaona niwakati mwafaka kuhakikisha kwamba tunatekeleza zile juhudi zote zilizofanywa katika 'kupromote Royal Tour' kwahiyo tunajitahidi sana kuielezea sekta ya Utalii na kuhakikisha kwamba tunawakaribisha wawekezaji wengi zaidi kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali kwenye sekta ya Utalii." Amesema Pendo

Amesema pia wanaitangaza sekta ya Elimu kwasababu kunaviwanda vinajengwa na watahitaji watanzania wenye uwezo wa kwenda kufanya kazi kwenye viwanda pamoja na kampuni za Uwekezaji.

Amesema kuwa miongozo mbalimbali ya TIC inatoa mwongozo zaidi katika kutangaza Sekta ya Elimu.

"Tunawaomba watanzania kuja banda la TIC kupata Elimu, hapa tunatoa elimu ya Uwekezaji, fursa zilizopo katika Uwekezaji, taratibu za kuweza kupata cheti cha Uwekezaji pamona na jinsi ya kujisajili na Kituo cha Uwekezaji." Amesema Pendo.

Amesema kuwa TIC inatoa huduma mahali pamoja ambapo taasisi za serikali 12 zineungana kwaajili ya kumsaidia mwekezaji .

Taasisi hizo ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania( TIC), taasisi inayohusika na Vibali vya kufanya kazi (Work Permity), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Wizara ya Ardhi, Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA).

Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Taasisi nyingine ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Uhamiaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...