Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe hivi karibuni ametembelea Kijiji cha Kidete katika Halmashauri ya wilayani ya Kilosa ili kujionea uharibifu wa kuta za bwawa la Kidete uliotokana na mvua za masika mwaka 2008.
Bwawa la Kidete kwa muda mrefu limekuwa likitumiwa na Wananchi kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji lakini tangu wakati huo, hakuna kilimo cha umwagiliaji kwa Wakulima wa eneo hilo.
Waziri Bashe akiwa ameambatana na Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi; Wananchi wa Kidete wamemwambia Waziri Bashe kuwa wameshindwa kulima kwa ufanisi zao la vitunguu maji ambavyo vimekuwa ni chanzo kikuu cha uchumi wao na kuuza katika nchi za Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wakulima hao pia, wamemweleza Waziri Bashe kuhusu changamoto ya kupanda kwa bei ya mbolea na kuwa chanzo cha kushindwa kuzalisha mazao ya chakula na biashara kwa tija.
Waziri Bashe amewaeleza Wakulima na Wananchi hao kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeichukua changamoto ya bwawa hilo na kuifanyia kazi; Ambapo amemuagiza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Mweli kukutana mara moja na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kukutana na kujadili namna ya kumpa kazi Mkandarasi anayejenga kipande cha reli ya SGR kutoka Kilosa (Morogoro) hadi Mpwapwa (Dodoma).
“Tutamuongezea wigo wa kazi, Mkandarasi anayejenga reli ya SGR ili ajenge na bwawa hili la Kidete; Kazi hii ya ujenzi wa bwawa italipwa na Wizara ya Kilimo kwenye bajeti ya mwaka 2022”.
#Ajenda1030 #kilimonibiashara
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...