
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk, Ashatu Kijaji, akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko Mkuu wa UTT AMIS, Mfaume Kimario, kuhusu fursa zinazotokana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango.
Naibu Gavana, Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Kassim Msemo (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa UTT AMIS, Rahim Mwanga (kushoto), alipofika kujionea huduma na elimu inayotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.


Afisa Masoko Mkuu wa UTT AMIS, Mfaume Kimario, akitoa maelezo kuhusu fursa zinazotokana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na kampuni ya uwekezaji ya UTT AMIS.
Afisa Uendeshaji wa UTT AMIS, Nuru Chimwenda, akitoa ufafanuzi kwa wateja waliofika katika Banda la kampuni hiyo katika viwanja vya Sabasaba.
Ofisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Doris Mlenge, akitoa maelezo kuhusu fursa zinazotokana na mifuko ya uwekezaji wa pamoja inayoendeshwa na kampuni ya uwekezaji ya UTT AMIS.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya UTT AMIS, Daudi Mbaga (wa tatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa UTT AMIS ndani ya banda lao katika maonyesho ya Sabasaba Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...