Jane Edward,Arusha


Wakulima wametakiwa kulima kilimo ikolojia kinacho lenga kuangalia ustawi wa kilimo ,mlaji ambazo zinalinda na kuheshimu mahusiano ya viumbe hai na mazingira ili kuwezesha matokeo chanya ya kiafya,kiuchumi,kijamii na kimazingira.


Hayo yamesemwa jijini Arusha na Meneja miradi kutoka shirika la Islands of Peace (IDP) ,Ayesiga Buberwa wakati akizungumza katika kongamano la wadau wa kilimo cha Ikolojia Arusha na kuwashirikisha wadau wa kilimo kutoka taasisi mbalimbali pamoja na wakulima .

Buberwa amesema kuwa, lengo la kongamano hilo linalenga kuhakikisha wadau wote wa kilimo wanakuwa na uelewa wa pamoja kuhusu dhana kuu ya kilimo cha ikolojia ambayo itawajengea uwezo wadau wa kilimo ikolojia katika kujenga hoja zenye mantiki wa utengenezaji wa mpango mkakati wa kilimo ikolojia ambayo huongozwa na kamati maalumu kutoka wizara ya kilimo na wadau mbalimbali.

Mkurugenzi wa shirika la IDP Tanzania,Ludovick Jolly amesema kuwa, wanataka kuhakikisha wakulima wanakitumia kilimo ikolojia kwani kinahifadhi mazingira na kuzalisha mazao mengi zaidi ambayo hayana madhara .

"Kilimo ikolojia ni kilimo ambacho kila mkulima anapaswa kukitumia kwa kuzingatia kuwa matumizi ya kilimo hicho yakitumika yataimarisha ardhi na mkulima kupata mazao mengi" Alisema Jolly

Naye Mtaalamu wa mbegu kutoka Mtandao wa Bayoanuai Tanzania (TABIO),Daud Manongi amesema kuwa,wanaendelea kuhamasisha kilimo hicho ili wakulima waendelee kutumia mbegu za asili na kuweza kuongeza kipato zaidi.

Mkurugenzi wa Island of Peace (IDP)Ludovick Jolly Akizungumza na wadau wa kilimo jijini Arusha.

Meneja miradi kutoa shirika la IDP Ayesiga Buberwa akifafanua umuhimu wa matumizi ya  kilimo cha ikolojia.
Washiriki wa Mkutano wakiangalia mazao.
Mkurugenzi wa IDP akifurahia jambo na wadau wa Kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...