Mkurugenzi wa KTO Maggid Mjengwa akikabidhi vitabu kwa Mkurugenzi wa TVET Dr Noel Mbonde Leo katika ukumbi wa KTO.Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa chuo Arnatouglu FDC, Victoria Isumbwa akipokea vitabu kwa niaba ya vyuo 13.

 

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) leo limekabidhi msaada wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa ajili ya washiriki wa programu ya Elimu Haina Mwisho (EHM) ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuendeleza maarifa kwa wanawake vijana waliokatishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali.

Vitabu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 70, vimekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa elimu na mafunzo ya ufundi (TVET) katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Dr Noel Mbonde, lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa vitabu vya kufundishia na kujifunzia, katika vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs).

Msaada huo unajumuishi Vitabu vya masomo ya sekondari, Miongozo na vitini vya kufundishia fani mbalimbali za ufundi kwa washiriki wa programu ya EHM, na masomo bebezi katika programu ya mafunzo ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM/ECD) au ualimu wa chekechea.

Jumla ya vitabu 3,195 vya masomo ya sekondari vikiwemo vya kiada na ziada vimetolewa kwa ufadhili wa Mastercard Foundation (MCF) kwa ajili ya vyuo 13 vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) ambavyo vimeanza kutekeleza programu ya EHM mwaka huu wa 2022. Vyuo hivi ni pamoja na Arnautouglu (Dar es Salaam), Bariadi (Simiyu), Buhangija (Shinyanga), Chala (Rukwa), Chilala (Lindi), Gera (Kagera) Kilosa (Morogoro), Kisangwa (Bunda), Msingi (Singida), Musoma (Mara),Nandembo (Ruvuma), Tarime (Mara) na Ulembwe (Njombe).

Vitabu vingine ni miongozo ya ufundishaji wa fani mbalimbali za ufundi kwa programu ya EHM katika vyuo 54 vya Maendeleo ya wananchi. Fani hizo ni Kilimo, Uashi, Ufugaji, Upishi wa vyakula, Ufundi wa magari, Ubunifu wa mavazi na teknolojia ya nguo, na Umeme wa majumbani. Kwa upande wa masomo bebezi kwa programu ya ECD ni pamoja na Ujasiriamali, Kompyuta, stadi za Maisha na Mawasiliano (Communication Skills) ambavyo vitakwenda kwa vyuo 10 vinavyotekeleza programu hiyo.

KTO inatoa shukrani za dhati kwa washirika wake ambao ni Mastercard Foundation na Serikali ya Sweden kupitia Shirika la Misaada la Maendeleo Sida, kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa hivi ambavyo vitasaidia kufikia malengo ya programu husika.

Zaidi ya wanawake vijana 2,000 wamejiunga na programu ya EHM mwaka huu wa 2022. Programu hii inalenga kuwawezesha wanawake vijana kufikia malengo yao kielimu kwa kuwapa fursa ya kurejea shuleni kupitia FDCs, ambapo wanasoma masomo ya sekondari kupitia mfumo usio rasmi, masomo ya ufundi, Ujasiriamali na stadi za Maisha.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...