
TAMASHA kubwa la kumtafuta Mama Ntilie bora kwa
mwaka 2022 linatarajiwa kufanyika Septemba mbili na tatu mwaka huu
katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam kwa mchuano mkali wa
Mama Ntilie watano kutoka katika Wilaya zote za jijini la Dar es Salaam
huku Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha tamasha hilo likitalofanyika Septemba 3.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijinii Dar es Salaam mwanzilishi na
Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanawake Jikoni Bussiness na
mwandaaji wa tamasha hilo Nice Mamuya amesema kuelekea kilele cha
tamasha la Mama Ntilie litakalofanyika tarehe 3 katika viwanja vya
Leaders jijini humo litakwenda sambamba na malengo ya taasisi hiyo kwa kuchochea fikra
za wanawake, kuamsha hali chanya ya maendeleo kwa wanawake pamoja
kuwajengea uwezo, maarifa, teknolojia na mitaji.
Amesema
tamasha hilo la
la Mama Ntilie limedhamiria kulitangaza kundi hilo na kuwa kundi rasmi
kama makundi
mengine yanayojihusisha na shughuli za ujasiriamali na litahudhuriwa
na vongozi wa Serikali, taasisi binafsi, wadau wa maendeleo na
wajasiriamali.
'' Kwa kushirikiana na Clouds Media tumeandaa tamasha hili pia kwa kuhakikisha kundi hili linakuwa zaidi...Wananchi tujitokeze katika siku ya kilele tarehe tatu kuanzia saa saba mchana na kushuhudia mambo makubwa yanayofanywa na kundi hili muhimu katika maeneo yote nchini'' Amesema.
Amesema,
wameanza tamasha hilo jijini Dar es Salaam na wataliendeleza katika
mikoa mingine ya Tanzania na kuwataka akina Mama Ntilie kujiandaa
kulipokea tamasha hilo katika mikoa yao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya Wanawake Jikoni Bussiness Sheree
Andersen amesema, kuelekea kilele cha tamasha hilo Mama Ntilie watafanya
mashindano siku ya tarehe mbili kwa kuwahusisha Mama Ntilie 5 kutoka
katika Wilaya zote za jiji la Dar es Salaam na mshindi atapatikana
kupitia mtihani na vitendo vya kazi na atatangazwa siku ya kilele na
kukabidhiwa zawadi kubwa ambazo zimetolewa na wadhamini.
Amesema
vigezo vilivyotumika kupata washiriki ni pamoja Mama Ntilie mtanzania,
mwenye umri wa miaka 18-35, usafi katika biashara, bei ya chakula, idadi
ya wateja anaowahudumia, sehemu anaponunua bidhaa pamoja na ubora wa huduma anayoitoa kwa wateja.
Akizungumza
kwa niaba ya kampuni ya Kilombero Sugar Company Limited kupitia bidhaa
ya Bwana Sukari mtafti wa masoko kutoka kampuni hiyo Lenin Rugaimukamu
amesema kampuni hiyo inatambua mchango wa akina Mama wajasriamali na
udhamini wao umelenga kushirikiana na kundi hilo la wajasiriamali muhimu
na watatoa bidhaa yao ya sukari ikiwa ni kiungo muhimu katika shughuli
zao za mapishi.
Pia
Maimuna Hassan ambaye ni Meneja Masoko wa Nice & Free Pads amesema
kampuni hiyo imedhamini kutokana na mchango mkubwa wa akina Mama Ntilie
katika kujenga uchumi na ndio watumiaji wakubwa wa bidhaa ya kampuni
hiyo na watatoa bidhaa hiyo ya Nice & Free Pads ili kuwaweka huru
na salama Mama Ntilie wakati wakitekeleza majukumu yao.
Pia
Evelyn Marriot kutoka Bongo Toothpick amesema wamedhamini tamasha hilo
la Mama Ntilie kutokana na umuhimu wa kundi katika jamii pamoja na ushirikiano
wanaoupata kutoka kundi hilo ambalo ni wateja wakubwa wa bidhaa zao
ambazo zinatengenezwa nyumbani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...