Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ameunga jitihada za
Rais Samia Suruhu Hassan za kuhimiza wananchi kujitokeza kushiriki zoezi la
sensa ya watu na makazi kwa kuandaa bonaza la michezo ya aina mbalimbali kwa
ajili ya kuhamasisha zoezi hilo.
Akizungumza wakati akifungua bonanza hilo linalofanyika Viwanja vya Shule
ya Sekondari ya Ikungi alisema limelenga kuunga jitihada za Rais Samia za
kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ambalo ni muhimu
kwa Taifa.
“Lengo la bonanza ili ni kuhamasisha wananchi wa Wilaya ya Ikungi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la sensa ya
watu na makazi litakalofanyika Agosti 23,
2022 ili waweze kuhesabiwa kwa maendeleo ya taifa na ili serikali iweze
kutupangia mipango mbalimbali ya maendeleo ni lazima tujitojeze kwa wingi kuhesabiwa
bila kukosa ” alisema Mtaturu.
Akizungumzia Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Mtaturu
alisema ni pamoja na kuisadia Serikali
kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo
ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa
ajenda za maendeleo za kimataifa.
Alisema taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika
utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi
husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali na kupata taarifa za
msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi
za mipango katika ngazi zote.
Aidha Mtaturu alisema umuhimu wa sensa hiyo ni pamoja na kigawio katika
kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira
na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi.
Pia alisema umuhimu wa sensa hiyo ni kupata taarifa itakayowezesha serikali
kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni
muhimu kwa usimamizi wa mazingira na msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa
demokrasia.
Alisema bonaza hilo ambalo limeanza leo limeanza kwa mashindano ya timu nne
za mpira wa miguu ambazo jumla yake zitakuwa nane na kuwa kesho itakuwa ni
kilele cha bonanza hilo ambapo kutakuwa
na michezo ya aina tofauti kama, mchezo wa bao, kuruka kamba kwa akina mama
‘malede’ mchezo wa bao, karata, Netball, kuruka kamba na mingine mingi na mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro.
Alizitaja timu zitakazoshiriki bonanza hilo kuwa ni Wakala FC, Sokoni FC,
Bodaboda FC, Golden Boys, Matongo FC, Choda FC, Mampando FC na Makiungu FC.
Alitaja zawadi kwa mshindi wa kwanza kwa mpira wa miguu kuwa ni Sh.300,000,
mshindi wa pili 200,000 na mshindi wa tatu ataondoka na kitita cha Sh.100,000.
Mtaturu alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki bonanza hilo la kuhamasisha zoezi kujitokeza kwa wingi na kufanikisha zoez la sensa ya watu na makazi 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...