
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Fatma Abubakar Mwasa leo 20 Agosti, 2022, ametembelea banda la TAWA katika viwanja vya Gymkhana Mkoani Morogoro ambako Mbio za riadha za 'Selous Marathon' zimefanyika.
Akiwa katika banda la TAWA, Mhe. Mwasa aliweza kupata maelezo mafupi kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na TAWA.
TAWA imetumia mbio riadha za 'Selous Marathon' kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika Pori la Akiba la Selous lililopo mikoa ya Lindi na Pwani, Pori la Akiba Pande lililopo jijini Dar es Salaam na Pori la Akiba Wamimbiki lililopo Mkoani Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...