Na Mashaka Mhando Tanga
RAIS Samia Suluhu Hassan, Jumatatu anatarajiwa kuzindua Chuo cha Kijeshi cha Maofisa Uhamiaji kilichopo wilayani Mkinga mkoani Tanga na kufunga mafunzo ya askari 818 waliopata mafunzo ya awali ya jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga, Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba alisema kwamba Rais anatarajiwa kuwasili Jumapili mchana mjini Tanga na kupatiwa taarifa ya mkoa kabla ya Jumatatu kuzindua chuo hicho kilichojengwa katika eneo la Boma-Kichakamiba.
Mkuu wa mkoa alisema baada ya kuzindua chuo hicho, atawatunuku maofisa na kuapisha askari wapya wapatao 818 waliofudhu kozi ya awali ya mafunzo ya uhamiaji.
Mkuu wa mkoa aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi Barabarani ili kumalaki Rais ambaye hii itakuwa mara yake ya kwanza kufanya ziara mkoani Tanga tangu awe Rais.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...