Na. Damian Kunambi, Njombe
Wananchi wa kata ya Nkomang'ombe iliyopo Wilayani Ludewa mkoani Njombe wamempokea mbunge wao kwa shangwe kutokana na kauli ya serikali juu ya ulipaji fidia kwa wananchi waliozunguka mradi wa liganga na Mchuchuma ambapo wamekuwa wakisubiri fidia za maeneo yao kwa zaidi ya miaka 7 pasipo kuyaendeleza.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na Wananchi hao mbunge JesephKamonga amesema kuwa suala hili la fidia kwa wananchi amekuwa akiliongelea sana bungeni na baadae walimwambia watakuja kufanya tathmini upya lakini hakuweza kukubaliana na hilo.
" Ndugu zangu hili jambo nimelizungumziq sana bungeni na wakaniambia watakuja kufanya tena tathmini lakini mimi nilikataa kwakuwa najua wengi wenu maeneo yamekwisha haribika na miti iliyokuwepo imeteketea kwa moto", Anesmema Kamonga.
Amesema kutokana na malipo hayo kuchukua muda mrefu amesema aliwasilisha ombi kwa serikali ili wananchi hao wa Liganga na Mchuchuma waweze kulipwa na riba ya kila mwaka ulio ongezeka tangu wafanyiwe tathmini.
Ameongeza kuwa serikali ya Rais Samia ni sikivu na inajali wananchi wake hivyo wananchi wanapaswa kujenga imani kwa Rais wao pamoja na chama cha mapinduzi.
Aidha kwa upande wa Mhandishi kutoka katika shirika la maendeleo la Taifa (NDC) Godfrey Mahundi ambaye alimuwakilisha mkurugenzi wa shirika hilo amesema tayari utaratibu wa kuhakiki majina ya walipwaji fidia umeandaliwa ambapo timu ya uhakiki itawasili mwezi ujao.
" Timu ya uhakiki itawasili mwezi wa tisa hivyo nawasihi kila mmoja awe na akaunti ya benki kwaajili ya kufanyia malipo na kwa atakayekuwa hana anapaswa kufungua kwakuwa malipo ya fidia yatafanyika kwa njia ya akaunti za benki", Amesema Mahundi.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na biashara Ashatu Kijaji akiwa mkoani Njombe katika ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan alisema kiasi cha sh. Bl. 16 tayari kimekwisha tengwa kwaajili ya ulipaji fidia kwa wananchi wa Liganga na Mchuchuma hapo mwezi Octoba mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...