WADAU wa masuala ya Semina za Jinsia na Maendeleo ( GDSS),wamedai kuwa ni muhim kuwepo na bajeti ambayo inatekeleza na kuzingatia usawa wa jinsi na Jinsia .

Hayo yalisemwa kwa nyakati tofauti na washiriki wa Semina za Jinsia na Maendeleo,ambazo semina hizo uratibiwa na TGNP Mtandao.

Katika mada iliyokuwa ikizungumzia uwezeshaji wa wanawake kupitia bajeti yenye mrengo wa kijinsia 

Juma Ally ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya kijamii,alisema kuwa umuhim wa kuwa na bajeti yenye mrengo wa kijinsia unasaidia kuwaondolea kero wananchi katika makundi yote maalum.

"Kutozingatia masuala ya mrengo wa kijinsia husababisha kero katika huduma za kijamii zikiwemo za afya,maji na nyingine nyingi," alisema.

Hamida Jamal mshiriki wa Semina za Jinsia na Maendeleo,alisema kuwa bajeti yenye mrengo wa kijinsia inazingatia upatikanaji wa fedha mgawanyo na mahitaji yaliyopo na nani yanamguza ,zaidi jamii inahitaji afya ,shule,maji na huduma nyingine muhimu.

Alisema katika huduma hizo mahitaji ya wanawake ni mengi zaidi kuliko wanaume ,hivyo bajeti ikizingatia mahitaji ya wengi itakuwa nirahisi kupunguza kero zinazowakabili wanawake.

"Kwa mfano katika shule wanafunzi wa kike wanatakiwa kuwa na matundu ya vyoo ya kutosha ,chumba cha kujihifadhi ,kuwe na taulo za kike na vilevile kuwepo na maji ya uhakika katika shule," alisema.

Idd Mziray ambaye anatoka katika shirika la Jinsia na ujana,alisema kuwa bajeti yenye mrengo wa kijinsia inatakiwa kuzingatia mahitaji ya makundi ya kijamii.

Alisema nchi inataja bajeti kila mwaka ,lakini bajeti pamoja na kutajwa bado kwa upande wa wanawake kumekuwa na changamoto kunufaika kupitia bajeti hizo.

" Ukiangalia bajeti ya kilimo imeongezwa kiasi kikubwa cha fedha,lakini pamoja na kuongezwa kiasi cha fedha watakaonufaika ni wanaume kwa sababu ndio wanaomiliki ardhi kwa asilimia kubwa tofauti na wanawake," alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...