Balozi wa China Nchini Chen Mingian akikabidhi Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk.Albina Chuwa Ua kuoyesha ushirikiano wa Tanzania na China anayeshuhudia ni Kamisaa wa Sensa Zanzibar Balozi Mohamed Haji Hamza.Mtakwimu Mkuu wa Serikali wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dk.Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

* Sensa ijayo kuwa na maswali 10 badala ya maswali 100

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema kuwa iko katika maandalizi ya mwisho ya kutoa matokeo sahihi ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika Agasti 23 mwaka huu .

Hayo ameyasema Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Zanzibar, Balozi Mohamed Haji Hamza wakati wa mkutano wa mashirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na China jijini Dar es Salaam.

Balozi Hamza amesema wapo katika maandalizi ya kutoa matokeo ya takwimu hizo za sensa ambazo ni muhimu katika kufanikisha maendeleo ya nchi.

“Sensa ina hatua tatu ambazo ni maandalizi ya kuhesabu, kuhesabu na baada ya kuhesabu pamoja hatua ya tatu ya kuhesabu kutoa matokeo ya kile tulichokifanya ili takwimu hizo zikatumike kufanikisha maendeleo ya nchi, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kabisa wasuburi na wakati ukifika watapata taarifa ,” amesema Balozi Hamza

Aidha Balozi Hamza amesema mashirikiano ya Tanzania na China yalianza toka miaka 60 iliyopita na katika Sensa ya mwaka huu China imehusika kutoa vifaa mbalimbali kufanikisha zoezi hilo ikiwemo vishikwambi na kompyuta mpakato.

“China wamekuwa pamoja na sisi katika kila hatua ya maendeleo ya nchi yetu tunawashukuru kwani kupitia wao na wadau wengine wamesaidia zoezi la sensa kwenda vizuri na kilichobaki ni muda ufike ili kuweza kutoa matokeo,” alisema

Naye Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk. Albina Chuwa ameiomba China kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha wanatengeneza miundombinu ya takwimu ili kurahisiha zaidi zoezi la sensa kwa miaka ijayo.

“Kama tutatengeneza miundombinu ya takwimu sensa ya miaka ijayo tutakuwa na maswali 10 badala ya 100 lakini pia itasaidia kuwa na mifumo ya kutoa takwimu kila siku, tunaendelea kuwashukuru ndugu zetu wa China ambao wanekuwa wakiunga mkono juhudi za Serikali yetu na sasa tutafanya mashirikiano kati ya NBD ya Tanzania na China,” alisema Dk. Chuwa

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingian alisema wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika mambo mbalimbali ya maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...