Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa  Uwekezaji  na Biashara nchini Exaud Kigabe  anayefuata ni Mkuu wa  Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele a na mwenye suti ni Afisa Msajlli BRELA Francis Filimbi akifafanua jambo.

Na Khadija Kalili, KIBAHA
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wameondoa changamoto ya wananchi kwenda katika ofisi za BRELA kufuata huduma kwa wao wenyewe kuitoa ya usajili kwa njia ya Mtandao kule walipo.

Maonesho yayo yalianza Oktoba 5 mwaka huu na kuzinduliwa na Rais wa Mstaafu wa awamu ya sita Mheshimiwa Jakaya Kikwete ambapo yaliwakutanisha wamiliki wa viwanda 200 vikubwa na vidogo.

Maonesho hayo yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kuratibiwa na Abubakari Kuenge kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO.

Huku wadhamini wakii wa ni Kongani ya SINO TAN, DAWASA, TIB,TANROAD na CAMAL GROUP.

Akizingumza kwenye hotuba ya kufunga na kutoa shukurani zake za dhati Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kunenge amewashukuru wadhamini wote ambao wamejitoa kwa hali na mali katika kufanikisha maonesho hayo.

"Nawapongeza sana wadhamini kwank wameleta mapinduzi makubwa ya maonesho hay ukilinganisha na yale yaliyofanyika katika miaka ya nyuma huku nikiwaahidi kuanzia mwakani tutafanya maonesho ya Kanda"amesema RC Kunenge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...