Na Khadija Kalili
 KIBAHA
NAIBU Waziri wa Uwekezaji Viwanda na biashara nchini mheshimiwa Exaud Kigabe amewataka Watumishi wa Idara ya Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi kutoa elimu kwa wananchi kwani wananchi wengi hawaelewi masuala ya upangaji wa matumizi ya ardhi.

Amesema hayo wakati alipopita katika banda la Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi lililopo Kibaha katika maonyesho ya tatu ya Uwekezaji na Biashara yanayoendelea katika viwanja vya maili moja standi kabla ya ufungaji wa maonyesho hayo yaliyofanyika kwa siku tano.

Amesema Watumishi hao waendelee kutoa elimu kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha kuhusu upangaji wa matumizi ya ardhi ili wajue kama maeneo yao yamepimwa au hayajapimwa na yapo katika matumizi gani ili hata sekta binafsi wakija kwa ajili ya uwekezaji wasipate taabu.

Aidha ameungumzia urasimu wa kutatua migogoro ya ardhi Mheshimiwa Kigabe alisema utatuaji wa migogoro usichukue muda mrefu nakusababisha Mwekezaji anaamua kuamia sehemu nyingine na wengine kususa kabisa.

Mheshimiwa Kigabe amemuhoji Kamishna Msaidizi wa Mkoa wa Pwani Hussein Iddi kwamba anatumia njia gani anatumia kutatua migogoro ya ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Pwani na kuwataka Watumishi hao kuwajibika kikamilifu kwa kutatua migogoro ya ardhi kwa haraka na kwa haki pasipo kumwonea mtu yeyote.

Kamishna Msaidizi wa Mkoa wa Pwani Hussein alisema tatizo lililopo ni kwamba wawekezaji wengi hupokelewa na mikono isiyo salama ya wauzaji wa ardhi na kujikuta wanaingia kwenye ardhi zenye migogoro kwa kununua ardhi kwa watu ambao sio wamiliki wa maeneo yao.

Amesema wanachofanya ni kutoa elimu ili kuitatua migogoro hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza mabaraza ya ardhi katika mkoa wa Pwani ambayo yanafanya kazi katika kata za mkoa huo kuwasaidia wananchi kutatua migogoro hiyo.
Naibu Waziri wa Uwekezaji  Viwanda  na Biashara nchini (kushoto)  Exaud Kigabe akiwa na  Kamishna Msaidizi Mkoa wa Pwani Hussein Sadiki Iddi alipotembelea kwenye banda la Wizara ya Ardhi Nyumva na Maendeleo ya Makazi  kwenye maonesho ya tatu ya Uwekezaji Biashara na Viwanda yaliyohitimishwa leo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Naibu Waziri wa  Uwekezaji na Biashara nchini Exaud Kigabe alipowasili hapa akisalimia Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...