Na Khadija Kalili
TAMASHA kubwa la vyakula vya kiafrika litakalofahamika kwa jina la 'African Cuisine Festival' 2022 kufanyika Oktoba 14 hadi 16 kwenye viwanja vya Ndoto Polepole Farm Mapinga Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mapinga Mratibu wa Tamasha hilo amesema Barozi wa Bodi ya Utalii wa Waafrika na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Emblem International Mariam Lesian.

Amesema nchi 30 zinatarajiwa kushiriki  nakukutanishwa pamoja katika kuonesha aina mbalimbali za vyakula vyao vya asili kutoka kwenye nchi zao.

Mariam amesema lengo la tamasha hilo ni kujivunia urithi wetu wa kiafrika pamoja na kudumisha umoja wa nchi zetu za kiafrika kwa kupitia vyakula vyetu, tamaduni zetu na vivutio vyetu vya utalii kwa ujumla.

Aidha amesema kuwa kutakuwa na kiingilio kwa madaraja mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...