Sabore Laiza, muhudumu wa afya ngazi ya jamii Ngorongoro Endulen akizingumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa tisa wa Afya (health Summit) leo Oktoba 12,2022 jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Amrefu Tanzania, Dkt. Frolance Temu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa tisa wa Afya ( Health Summit) leo Oktoba 12,2022 jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wahudumu wa ngazi ya jamii.

WAELIMISHAJI rika kwenye jamii wapewe nguvu ili kuendelea kutoa huduma kwenye jamii na kusaidia wananchi kuzidi kupata elimu ya afya.

Waelimishaji rika hao ambao ni wanasaidiwa na shirika la Amref Afrika ili kusaidia kuwapunguzia mzigo watoa huduma wachache kwenye jamii ambao wanazidiwa wingi wa wagonjwa.

Hayo yamesemwa na Dkt. Florence Temu Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania katika katika Kongamano la tisa la Afya (Tanzania Health Summit) 2022 linalofanyika katika Ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. amesema kuwa wahudumu hao wanatambulika na mfumo wa serikali pia wanatambulika na mifumo ya kimila katika maeneo yao.

Amesema kuwa wahudumu hao wanawapa elimu juu ya maradhi mbalimbali na namna ya kuchukua tahadhari pamoja na kutoa elimu ya kujikinga na magonjwa hayo na hasa ya mlipuko.

Amezitaja faida za kuwatumia waelimashaji rika kwenye jamii na kueleza kuwa kwa mwaka wanawafikia moja kwa moja watu takribani milioni sita.

“Matokeo tunayoyapata kupitia hawa waelimishaji rika kwa mwaka tunawafikia watu takribani milioni tatu mpaka milioni sita lakini kupitia kwa tunaita indirect tunawafikia watu milioni 15 kwa hiyo hawa watu muhimu kwenye kutoa elimu ya afya.” Amesema Temu

Neema Waziri Fundi Mwelimishaji rika katika Halmashauri ya Dodoma amesema kuwa yeye anawaelemisha vijana na wanawake waliojifungua katika masuala ya afya.

Ameeeleza changamoto ambayo inawakabili wanajamii “mimi nafanya kazi na vijana changamoto kubwa ambayo naiona kwenye bima ya afya ni kwamba hakuna muitikio mkubwa wa kuhakikisha kuwa kila mtu anakuwa na bima ya afya kwa sababu watu wanashindwa kumudu gharama kutokana na hali ya maisha au tamaduni ya famili yake ili kufanikisha jambo hili kwa pamoja elimu izidi kutolewa na kutoa faida za bima ya afya” .

Amesema kuwa Elimu isambazwe chini kwa sababu watu wanadhana kuwa matajiri pekee yao ndio wanatakiwa kuwa na bima ya afya ilhali dhana hiyo ni potofu kwa kuwa mtu yoyote anaweza kuugua.

Naye Masai amesema kuwa changamoto ambayo inaikumba jamii yake ya wafugaji ni kuhamahama kwenye makazi yao jambo ambalo linapelekea kuwa mbali na huduma za afya.

“Changamoto iliyokuwepo sisi ni wafugaji wa mifugo ambapo tunahamahama tukifuata malisho kwa hiyo wananchi wanaweza kuacha lile eneo la Hospitali kwa ajili ya kufuata malisho wakaenda na Watoto kule ilhali hospitali haihami kwa hiyo umbali wa kupata huduma za afya unaongezeka.”

Alipoulizwa kuhusu maboresho ya bima ya afya kwa wote amesema kuwa hata vijijini huduma ya Bima ya Afya inatumika ijapokuwa kuna changamoto ya kutokubalika kwa bima ya afya ya NHIF kwenye kituo cha afya cha Endreni, na kwamba huduma hiyo inapatikana kwenye zahanati pekee.

“Serikali ijikite kwenye kuongeza vituo vya afya na kutoa elimu kwa watu wa vijijini wajue umuhimu wa bima ya afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...