
Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel akimkabidhi ngao kutambua mchango wa Mradi wa HPSS kwa Meneja Mradi Ally Kebby kwenye mkuatano wa Tanzania Health Summit, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Profesa Abel Makubi akizungumza katika mkutano wa Tanzania Health Summit jijini Dar es Salaam.
Rais wa Tanzania Health Summit Dk.Omary Chillo akitoa maelezo kuhusiana na malengo ya mkutano wenye kwenda kuboresha huduma za afya nchini, jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja wadhamini wa Tanzania Health Summit na Mgeni Rasmi Naibu Waziri Afya Dk.Godwin Mollel katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha mbalimbali za matukio kwenye mkutano wa Tanzania Health Summit unaoendelea jijini Dar es Salaam.
*Mradi wa HPSS wadhamini Mkutano wa Tanzania Health Summit.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
NAIBU Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel amesema serikali îmewekeza katika sekta ya afya katika maeneo ya miundombinu , vifaa tiba pamoja wataalam wa sekta hiyo lengo kutoa huduma bora za afya.
Dk.Mollel ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Afya Nchini (Tanzania Health Summit) alipomwakilisha Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango amesema mkutano huo una umuhimu katika kwenda kuboresha maeneo mbalimbali kutokana na mijadala itakayoibuliwa ndani ya mkutano huo.
Amesema kuwa licha ya kutoa huduma bora za afya nchini wataalam wenye shahada ya Udaktari kwenda vijijini ambapo huko ndio wananchi wengi na wanahitaki wataalam hao.
Dk.Mollel amesema kuwa katika majadiliano hayo kuweka suala hilo kwa madaktari wenye shahada kwenda kutumika vijijini kutokana na serikali kuweka miundombinu wenzeshi wa kufanya wataalam hao waishi katika maeneo hayo.
Aidha amesema mkutano huo ulete tija kwa kutoa mapendekezo mbalimbali ikiwemo na ile ya kisera ambayo itasaidia kufanya maboresho kwenye maeneo yenye changamoto ya utoaji wa huduma za afya nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk.Abel Makubi amesema kuwa kuna sheria imepelekwa bungeni ya kuwa na bima ya afya kwa wote ambapo mkutano huo ni sehemu ya kujadili eneo hilo.
Dk.Makubi amesema kuwa nchi ilipita katika mtikisiko wa ugonjwa wa Korona ambapo serikali iliweka jitihada kuboresha miundombinu ya katika hospitali , Vituo vya Afya pamoja na Zahanati ili kuhakikisha watanzania wanapata huduma za afya bora.
Amesema kuwa sasa kuna ugonjwa wa Ebola uko katika nchi jirani hivyo hatua zote zimeanza kuchukuliwa katika kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini.
Amesema licha kuwepo kwa huduma changamoto zipo ambapo kama wataalam kuendelea kufanya ubunifu wa utoaji huduma ikiwemo na utafiti.
Rais wa Tanzania Health Summit Dk.Omary Chillo amesema mkutano huo ni wa tisa utajadili mada mbalimbali na mafanikio yaliyotokana na wadau baada ya mikutano iliyopita katika maada 40 zitakazowasilishwa.
Amesema kuwa mkutano huo ni fursa ya kujifunza vitu vingine kwa wadau kwa kazi walizofanya na zilizoleta matokeo chanya kwenye sekta ya afya nchini.
Mkutano huo unakwenda na kaulimbiu ya “Ubora wa Huduma ya Afya Tanzania: Hali ya Sasa na Maboresho yanayohitajika ili kutekelezaMpango Mkakati wa Sekta ya Afya wa Tano (HSSP V)”, wadau katika mkutano huo watajadilihali ya sasa na maeneo ambayo yatahitaji rasilimali na jitihada zaidi ili kutimiza malengo.
Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya, unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi na kutekelezwa na Taasisi ya Uswisi ya Tropical and Public Health Institute ni miongoni mwa wafadhili wakuu wamkutano huo.
Meneja wa Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya Ally Kebby wa HPSS amesema mradi huo unalenga katika kuendeleza juhudi za ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora za afya kwa Watanzania.
"Wakati wa mkutano huo, mradi wa HPSS Tuimarishe Afya utaelezea mchango wake katika kufanikisha mpango mkakati wa Sekta ya Afya wa Tano (HSSP V)kupitia ubunifu wa mradi, hususan Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa) na mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa bidhaa za afya (Jazia Prime Vendor System)", amesema Ally Kebby,Meneja wa Mradi wa HPSSTuimarishe Afya.
Kebby amesema zaidi ya hayo, mradi wa HPSS itawasilisha matokeo yake mbalimbali ya utafiti ambayo yanatoa ufahamu katika mbinu zake zakusaidiautekelezaji wa HSSP V kwenye kongamano hilo.
“Kutekeleza Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya Tanzania: Uliopita na michango ya sasa ya Mradi wa ushirikiano kati ya Serikali za Uswisi na Tanzania wa HPSS Tuimarishe Afya”
Amesema katika mkutano HPSS pia utatoa picha zaidi ya mawasilisho 100 ya matokeo ya tafiti za mashirika mbalimbali kuhusu afua mbalimbali za afya.
Amesema mkutano huo utaingia katika agenda ya Mkutano wa 23 wa Pamoja wa
Mapitio ya Kiufundi ya Sekta ya Afya utakaofanyika mwezi Novemba 2022 na Mkutano wa Mwaka wa Mapitio ya Sera ya Sekta ya Afya utakaofanyika mwezi Desemba 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...