MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewataka wataalamu wa afya nchini kutoa michango yenye tija ya kuboresha mfumo wa afya kwa kuzingatia mpango wa Bima ya Afya kwa wote ambayo muswada wake ulisomwa kwa mara ya kwanza Bungeni hivi karibuni.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel alipomwakilisha Makamu wa Rais wakati wa ufunguzi wa kongamano la tisa la Afya Tanzania health Summit) linalifanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wataalamu wa afya kutoka sekta za umma na binafsi.

Dkt. Mpango amesema iwapo utaalamu utatumika na kuhamasisha watu kujiunga na bima ya afya Taifa litafikia lengo la matamanio ya kuboresha sekta ya afya kupitia mpango huo wa bima ya afya kwa wote.

Baada ya kuwasilisha ujumbe wa Dkt. Mpango, Dkt. Mollel aliwataka washiriki kujadili changamoto mbalimbali katika sekta hiyo na kutoa njia ya kusonga mbele.

"Wadau tutoe maoni kuhusu huduma ya afya Lakini, unapojadili kuhusu bima ya afya inayotarajiwa kuwa kwa wote, tunapaswa pia kujadili masuala ambayo yanaweza kusababisha kuzorota kwa Mfuko wetu wa Bima ya Afya (NHIF)..Kama NHIF itaporomoka ubora wa huduma za afya pia zitaporomoka, kwa hivyo tujadili namna kufanya NHIF kuwa endelevu," amesema.

Dkt. Mollel amewataka wataalamu hao pia kujadili suala la gharama za huduma za afya, akibainisha kuwa baadhi ya watoa huduma wanataka kupata faida kubwa.

"Tunapaswa kufikiria kuboresha mfumo wa afya sio biashara, haswa tunapojadili kuhusu mpango wa bima ya afya kwa wote." alisema.

Kaulimbiu ya mkutano ni 'Ubora wa Huduma ya Afya Tanzania: hali ya sasa na maeneo ya kuboreshwa kuelekea kufikia malengo ya Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya (HSSP V 2021-2026.)

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Abel Makubi amesema kuwa ubora wa huduma za afya ndiyo ajenda kuu ya Serikali, na wadau wengi wameunga mkono na kutoa maoni.

“Suala la huduma bora lisiwe kwenye utoaji wa matibabu pekee bali lianzie mafunzo ya kada hiyo vyuoni,” alisema.

Alisema kwa kipindi cha miaka 10 Serikali imefanya maboresho makubwa katika sekta ya afya na kuwataka wadau kuendelea kuunga mkono jitihada hizo.

Kwa upande wake, Rais wa Tanzania Health Summit Dkt.Omary Chillo amesema katika kongamano hilo mada mbalimbali zitajadiliwa na mafanikio yaliyotokana na wadau baada ya mikutano iliyopita katika mada 40 zitakazowasilishwa.

Ameongeza kuwa mkutano huo pia ni fursa ya kujifunza vitu vingine kwa wadau kwa kazi walizofanya na zilizoleta matokeo chanya kwenye sekta ya afya nchini.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Afya unaoendelea kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Tanzania Health Summit Dk.Omary Chillo akitoa maelezo kuhusiana na malengo ya mkutano wenye kwenda kuboresha huduma za afya nchini, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel  akiteta jambo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Prof. Abel Makubi wakati Mkutano Mkuu wa Afya wa 2022 (Health Summit 2022) unaoendelea kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akikabidhi zawadi wa taasisi shiriki za Mkutano Mkuu wa Afya wa 2022 (Health Summit 2022) unaoendelea kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano Mkuu wa Afya wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...