Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ally Hamis akionesha tuzo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyokabidhiwa na Taasisi ya Ustawi wa Jamii Wakati wa Mahafali ya 46 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Desemba 8, 2022.

*Watambua Mchango wake wa Kuanzisha Wizara ya Ustawi wa Jamii
* Wahitimu wapongezwa

TAASISI YA Ustawi wa Jamii (ISW) imetoa tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mchango wake kuimarisha Ustawi wa jamii ya Watanzania.

Tuzo hiyo imetolewa wakati wa Mahafali ya 46 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Novemba 8, 2022 ambapo wahitimu 3,234 wamahitimu masomo kwa mwaka wa Masomo 2021/2022.

Akizungumza wakati wa Mahafali hayo Mwenyekiti wa bodi ya Magavana ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Sophia Simba amesema kuwa wanatambua kuwa Rais Dkt. Samia kuwa ni mwana ustawi wa Jamii namba moja (1) kwa juhudi zake za kuhakikisha fani ya ustawi wa jamii inapewa msukumo mkubwa ili kuendelea kuibua na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania.

Amesema imedhihirika wazi pale ambapo alianzisha Wizara maalum ya kushughulikia masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kupinga ukatili wa kijinsia na watoto, kuboresha hali na maisha ya wazee na kuhakikisha wanawake wanapewa nafasi ya kushiriki na kutambuliwa mchango wao kisiasa na kiuchumi.

Kwa Upande wa Mgeni Rasmi ambaye ni Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ally Hamis amesema kuwa amefarijika kusikia juhudi mbalimbali zinazochukuliwa za kuongeza na kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia kama vile ujenzi wa madarasa na ofisi.

“Hatua hizi zinaendana na kile tulichoahidi bungeni kwenye hotuba ya bajeti kwamba tutaweka mazingira bora ya ufundishaji na kujifunza katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii ili kutoa mafunzo yanayokidhi mahitaji ya soko.” Amesema Mwanaidi Ally Hamis

Licha ya hayo amesema kuwa Wizara imepokea changamoto ya Hosteli na itaendelea kuifanyia kazi kwa kutenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Wakili Amon Mpanju, ameipongeza Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa mchango wao mkubwa katika jamii kwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma mbalimbali ikiwemo msaada wa kisaikolojia kwa Wananchi Msomera, Wahanga wa majanga ya moto katika soko la Karume na Mbagala na mafunzo mbalimbali juu ya afya ya akili ambayo imekuwa changamoto kubwa nchini na Dunia kwa ujumla.

Kwa Upande wa Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dkt. Joyce Nyoni amesema kuwa Katika fani ya Ustawi wa Jamii, jumla ya wahitimu 1,246 wamefaulu. Miongoni mwao, wahitimu 937 sawa asilimia 75 ni wanawake na wahitimu 309 sawa na asilimia 25 ni wanaume.

Katika fani ya Menejimenti ya Rasilimali Watu, jumla ya wahitimu 977 wamefaulu. Kati ya hao, wahitimu 731 sawa na asilimia 75 ni wanawake na wahitimu 246 sawa na asilimia 25 ni wanaume.

Katika fani ya Mahusiano Kazini na Menejimenti ya Umma imetoa jumla ya wahitimu 302. Kati ya hao, wahitimu 142 sawa na asilimia 47 ni wanawake na wahitimu160 sawa na asilimia 53 ni wanaume.

Katika fani ya Uongozi wa Biashara, jumla ya wahitimu 279 wamefaulu. Miongoni mwao wahitimu 165 sawa na asilimia 59 ni wanawake na wahitimu114 ambao ni asilimia 41 ni wanaume.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...