
Na Mwandishi Wetu
WAKATI Watanzania wakielekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka za Chrismas na Mwaka Mpya Kampuni ya Simu ya TECNO imewashauri kununua simu za Camon 19 au Spark 9 ili waweze kujishindia pikipiki mpya.
Taarifa ya kampuni ya TECNO wakati wa uzinduzi wa rasmi wa Promosheni ya Zigo la Desemba imeeleza hatua kwa hatua namna ya kujishindia Pikipiki mpya baada ya kununua Camon 19 au Spark 9 katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka 2022 huku swali kubwa likiwa ni zawadi gani utampa umpendae au kujizawadia mwenyewe kwa kuumaliza mwaka 2022 salama.
“TECNO imekujia na Zigo la Disemba ndani ya Mwezi huu wote ambapo mteja wetu ukinunua simu zetu anajishindia Pikipiki pamoja na zawadi nyengine kibao. Kampuni ya simu TECNO ilizindua rasmi promosheni ya Zigo la Disemba tarehe moja ya mwezi huu hadi sasa wateja wa TECNO wamejishindia TECNO Camon 19 na Spark 9 katika week ya kwanza ya promosheni hii lakini pia wameingia katika droo kubwa la Mwisho wa Mwezi la kushindania Pikipiki.”
Kwa mujibu wa Kampuni ya Simu ya TECNO ni kwamba wateja ambao wanapata nafasi yakujishindia zawadi hizo ni wale wanaonunua TECNO Camon 19 au Spark 9 ndani ya kipindi hiki cha promosheni ya Zigo la Disemba, vile vile zawadi nyengine kama earphone, Mabegi na Miamvuli yenye nembo ya TECNO zimekuwa zikitolewa papo kwa hapo.
Hivyo imeendelea kuwahimiza na kuwashauri wateja wao na Watanzania kwa ujumla kununua TECNO Camon 19 au Spark 9 wafurahie uwezo mkubwa wa camera ya MP64, battery ya mAh5000 na kioo kipana chenye kuchukua matukio mahiri ya picha na video katika msimu huu wa sikukuu.
“Tunaomba muendelee kutembelea kwenye maduka yote ya simu yenye promosheni Dar es Salaam na mikoani ili kujishindia zawadi tajwa. Au unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba za simu 0744545254, 0678035208 au tembelea @tecnomobiletz twitter, @tecnomobile facebook au @tecnomobiletanzania IG.”imesema taarifa hiyo kuhusu promosheni inayoendelea ya Zigo la Desemba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...