Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano, TPDC, Marie Msellem akizungumza na waandishi wa habari katika Jengo la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika maonyesho ya bidhaa za viwanda Tanzania yanayoendelea Kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Petro Kileo Kutoka Mkondo wa Juu TPDC, akizungumza na waandishi wa habari katika Jengo la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika maonyesho ya bidhaa za viwanda Tanzania yanayoendelea Kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Jengo la TPDC
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema matumizi ya gesi asilia majumbani, viwandani na kwenye magari vimechangia kupunguza uharibifu wa mazingira na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Aidha, limesema tangu mwaka 2004 hadi 2021 fedha za kigeni zaidi ya Sh. trilioni 60 zimeokolewa kutokana na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia majumbani, viwandani na kwenye magari.
Akizungumza leo katika maonesho ya saba ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa TPDC, Marie Msellemu amesema kuwa mpaka sasa shirika hilo limeunganisha gesi asilia katika viwanda 48, magari zaidi ya 1,400, nyumba 1,500, taasisi saba za Dar es Salaam na Mtwara na inatumika kwa asilimia 75 kwenye umeme.
Amesema kuwa wamekuwa wadau wa viwanda kwa muda mrefu na kwamba wanaendelea kuhamasisha matumizi ya gesi asilia kwa kuwa ni gharama nafuu inayoanzia Sh 1,000 kwa familia ya watu sita.
Msellemu amesema gesi asilia ni nishati na malighafi nzuri ya kutumia kwa sababu hupunguza matumizi ya nishati za mafuta mbadala ikiwemo petroli, dizeli, kuni na hivyo kusaidia utunzaji wa mazingira unaosababisha ukame.
"Tunashiriki katika maonesho ya viwanda kwa sababu wadau wetu wakubwa wapo hapa na lengo ni kupokea maoni ya wadau wanahitaji nini na tufanye maboresho gani. Niwahakikishie kiwa gesi asilia ni nafuu tofauti na matumizi ya nishati mbadala za mafuta ," Amesema.
Ameongeza kuwa wameunganisha nishati hiyo katika maeneo mbalimbali ya Mkuranga mkoani Pwani na Dar es Salaam (Sinza, Coca-Cola, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na nyumba za polisi Kilwa).
Pia amesema wanatoa huduma ya kushindilia gesi asili (CNG) katika vituo vya Ubungo na Tazara na kwamba wamiliki wa viwanda walio nje ya mradi wanatakiwa kuwasiliana nao kwa lengo wafikishiwe gesi hiyo kwa mitungi.
Amesisitiza kuwa mpango wa kujenga vituo vya kushindilia gesi katika maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Kairuki Pharmaceutical Industry Limited Zegeleni Kibaha na Soko la Samaki feri unaendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...