Na Avila Kakingo, Michuzi TV
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (HLRC), kimetoa wito kwa Serikali, kupitia Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, kuhakikisha sheria za kazi zinatekelezwa kikamilifu ili kuhakikisha wafanyabiashara wanazingatia sheria na viwango vya kazi na haki za binadamu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa (HLRC), Anna Henga wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 74 ya Haki za Binadamu yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Desemba 8, 2022 amesema Mashirika ya kiraia na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kuwafikia wafanyakazi na waajiri kuwahamasisha kuhusu kazi na haki za binadamu za pande zote mbili katika azma ya kukuza haki za binadamu katika sekta ya biashara.
Pia amesema Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria na Wizara ya Mambo ya Nje, kuridhia Itifaki ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu wa Haki za Watu Wenye Ulemavu Barani Afrika wa 2018. Aidha kuridhia Itifaki ya Mkataba wa Kimataifa wa kupinga unyanyasaji wa kingono sehemu za kazi( ILO Convention on sexual harassment in the place of work).
Hata hivyo Wakili Anna Henga amesema kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha kuwa tunalinda na kutetea haki za binadamu nchini.
"Wananchi kwa ujumla tunao wajibu wa kuheshimu haki za wengine, Viongozi wa dini wanabeba jukumu kubwa zaidi la kutoa elimu kwa waumini wake juu ya umuhimu wa haki za kila mmoja.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora (THBUB),Patient Ntwina akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 74 ya Haki za Binadamu amesema Pamoja na kauli mbiu ya Mwaka huu ys kuchagiza Utu na Haki za Binadamu kwa wote ni Vema kuwa na tahadhari na kusahihisha dhana potofu katika jamii kwamba haki za binadamu zinapaswa kufurahiwa bila kuzingatia mipaka.
Kwa upande wa Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Charlotta Ozaki Macias amesema kuwa harakati za kupigania haki za bianadamu zinafanana duniani Kote hivyo ameishauri serikali kufungua milango kwaajili ya majadiliano kuhusu marekebisho ya katiba yanayoweza kutatuachangamotio kama vile Tume huru ya Uchaguzi ambayo inafanya kazi kwa misingi ya utawala wa sheria.
Kwa Upande wa Mwakilishi wa Kikanda wa Umoja wa Mataifa amesisitiza Kila mmoja anatakiwa kuheshimu haki za binadamu Kukinga au kuzuia Kuvunja haki za Binadamu na kutangaza ili ziweze kufahamika kwa kila mtu.
Kwa Upande wa Mdau wa Haki za binadamu kupitia Viongozi wa Dini, Amesema kila mmoja ashike nafasi yake hasa kufuata maandiko matakatifu ili kulinda haki za binadamu. Pia amesema kuwa Kila mmoja ampende mtu mwingine kama vile ambavyo yeye anajipenda bila kudhuru haki ya kuishi pamoja na kuchagua chaguo lililo jema ambapo hakuna mtu anakatisha uhai wa mtu mwingine.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora (THBUB),Patient Ntwina akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 74 ya Haki za Binadamu yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Desemba 8, 2022
Mkurugenzi Mtendaji wa (HLRC), Anna Henga akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 74 ya Haki za Binadamu yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Desemba 8, 2022.

Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Charlotta Ozaki Macias akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 74 ya Haki za Binadamu yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Desemba 8, 2022
Baadhi ya wadau wa Haki za Bianadamu wakiwa katika mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 74 ya Haki za Binadamu yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Desemba 8, 2022
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...