
Waziri wa Nishati Januari Makamba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana usafirishaji wa mafuta ya Dizeli kwenda nchini Zambia mara baada kikao kati ya Tanzania wa Zambia kwa Wizara za Nishati, Ulinzi na Mambo ya Ndani , jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati nchini Zambia Mhandisi Peter Kapala akizungumza kuhusiana na makubaliano ya utekelezaji wa Bomba la Mafuta ya Dizeli kwenda nchini humo.
Waziri wa Ulinzi Nchini Zambia Ambrose Lufuma akizungumza kuhusiana na mikakati ya ulinzi wa bomba la mafuta ya Dizeli kwenda nchini Zambia yakitokea nchini Tanzania.

Picha mbalimbali za mkutano wa kujadili usalama wa bomba la mafuta ya Dizeli  kutoka Tanzania kwenda Zambia.
*Tanzania kunufaika na Uuzaji wa Gesi nchini Zambia
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SERIKALI ya Tanzania na Zambia yapitisha mapendekezo ya   kuimarisha  ulinzi wa bomba la Mafuta la Tanzania na Zambia (TAZAMA) ya usafrishaji wa mafuta ya dezeli na kuachana na usafirishaji wa mafuta ghafi yasiosafishwa.
Ulinzi huo unakwenda kutokana na usafirishaji huo unaweza kuhujumiwa na wananchi kwani hayo mafuta yakitolewa kwenye bomba yanakwenda katika matumizi tofauti na usafirishaji wa mafuta ghafi yasiosafishwa.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nishati Januari Makamba amesema nchi ya Tanzania na Zambia zina mradi wa muda mrefu ulioanzishwa na Marais Waanzilishi wa nchi  zote mbili Keneth  Kaunda na Rais Julius Kambarage Nyerere kuanzisha  bomba hilo la mafuta.
Amesema katika kufanya ulinzi huo kutakuwa  na walinzi kwanza na kufatia  teknolojia mbalimbali ikiwemo  Drone na Kamera za CCTV pamoja na elimu ya ulinzi kwa wananchi wanaopitiwa na bomba hilo kuwa sehemu ya ulinzi.
Pia nchi hizo zimekubaliana kuweka ratiba ya utekelezaji wa mapendekezo hayo yaliyotolewa na Wataalam wa nchi zote mbili, ndani ya siku 45 yawe yametekelezwa
Makamba alisema miaka ya  nyuma Bomba hilo la mafuta lilikuwa linasafirisha mafuta ghafi yasiyosafishwa na kuelekea nchini  Zambia ambapo huko kuna mtambo wa kuyasafisha mafuta hayo ili yawe mafuta safi na kuwa tayari kwa kutumia katika magari na mitambo mingine.
Makamba amesema Kutokana na maendeleo ya uchumi kati ya nchi mbili na Teknolojia kukua Serikali ya Zambia iliamua kubadilisha bomba la TAZAMA  kuacha kusafirisha mafuta ghafi na kutaka kuanza kusafirisha mafuta ya diseli na kutokana na hali hiyo walianza kufanya manunuzi ya kuwezesha bomba hilo kubadilishwa na imechukua gharama kubwa.
‘’Usafirishaji wa  mafuta ya  diseli  kwa njia ya bomba kunahitaji usalama wa bomba hilo  kuwa mzuri na kuwa makini nalo kwa sababu mafuta  yale ghafi ni mazito machafu ambapo hata kama   mtu  akiiba kwa kuchepusha bomba  hawezi kuyafanyia chochote tofauti na haya ya Diseli ambayo iko safi ,’’amesema Januari
Amesema bomba litakapochokonolewa na watu kuchepusha mafuta hayo ni hatari kubwa  hivyo nchi zote  tumeamua kufanya utaratibu wa usalama wa bomba na kutembelewa na na Mawaziri Waziri wa Nishati wa Zambia,Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya ndani wa Zambia  pamoja na wataalamu wao wakiwemo makatibu wakuu wa wizara hizo na wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi mbili kujadili kwa kina juu ya usalama wa bomba hilo na kutoa mapendekezo yatakayotuongoza katika kufanikisha jambo hilo.
Amesema hatua ya Zambia kubadilisha matumizi ya bomba hili kutoka kutumika kusafirisha mafuta ghafi hadi kufikia mafuta ya Diseli ni maamuzi makubwa  na ya msingi na kufanya Tanzania kuendelea kuwa soko  na njia ya kuhakikishia Zambia kuwa na  usalama wa mafuta na Bandari kutumika.
Kwa Upande wake Waziri wa Nishati nchini Zambia,Eng Peter Kapala aliishukuru Serikali ya Tanzania katika mkutano huo na kusema kuwa ni muhimu kutekeleza mapendekezo hayo kwa muda waliojiwekea.
Alisema ni jukumu la nchi zote mbili kuhakikisha usalama unakuwepo katika bomba hilo ili kusiweze kutokea kwa uharibifu wowote na kuhakisha uimarishaji wa ulinzi.
Waziri wa Kapala  amesema mbali na bomba hilo pia wanatarajia kununua gesi kutoka nchini Tanzania kwa kuwa na bomba lingine tena kutokana kuweka na uharibibifu wa mistu yanayochangiwa na matumizi nishati ya kuni.




.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...