*Aahidi kutumikia waledi nafasi hiyo

Na Mwandishi Wetu.
KADA Mbobevu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Chacha Wambura amesema kuwa ana imani na wajumbe wa CCM kumchangua katika kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu kwenye nafasi 20 Tanzania Bara.

Wambura ameyasema hayo kwa njia ya simu kuhusiana na uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) utaofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma.

Amesema kuwa ameanza kukitumikia Chama kwa muda mrefu na kushika nafasi mbalimbali ambazo ameweza kuzimudu kwa uaminifu na na maarifa yake ya kufanya chama kisonge mbele.

Wambura amesema kuwa wajumbe wamchague katika nafasi kati 20 ili kuweza kufanya mambo tofauti katika kushauri chama ndani ya wajumbe wenzake watakaochaguliwa.

"Nina uwezo wa kutosha katika kutumikia Chama hiki kwa nafasi niliyoiomba kuitendea haki imani yangu iko kwa wajumbe kunipigia kura ya ndiyo"

Mbali na kuwa Mwana CCM Wambura ni Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ua WAJA Group na kuamini kuwa anatosha kwenye nafasi hiyo.

Ameshukuru atika mkutano jina lake kurudishwa Kamati Kuu na anachosubiri kwa sasa ni kura za wajumbe kumpigia kura kuendeleza gurudumu la CCM.

WAJA ni mwekezaji kwenye viwanda vya chuma kupitia Waja Mabati, Uchimbaji wa Madini pamoja na sekta ya Elimu ambapo ana shule ya Waja Boys, Girls na Primary schools . Pia amewekeza kwenye sekta ya afya ambapo ana vituo vya afya, pamoja na Waja Hospitali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...