Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Aboud (aliyesimama) akifungua mkutano wa utoaji elimu kwa watumishi kuhusu Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya Kwa Wote, uliofanyika Januari 24, 2023 NIMR makao makuu, jijini Dar es Salaam.

Utoaji huo wa elimu ulilenga kuwapa uelewa watumishi kuhusu Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote ili wawe mabalozi wazuri katika kuelimisha makundi mbalimbali ya Jamii.

Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa Bungeni mwezi Februari mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said Aboud (aliyeketi katikati) akijibu maswali ya Watumishi wakati wa mkutano wa utoaji elimu kwa watumishi kuhusu Muswada wa Sheria ya  Bima ya Afya Kwa Wote uliofanyika Januari 24, 2023 NIMR makao makuu, jijini Dar es Salaam.


Muelimishaji kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) ambaye ni Afisa Mawasiliano Mtafiti Bwana Hamza Mwangomale, akitoa elimu kwa watumishi wa NIMR kuhusu Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya Kwa Wote. Mkutano huo wa utoaji elimu ulifanyika Januari 24, NIMR makao makuu jijini Dar es Salaam.









Watumishi wa NIMR wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kuhusu Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote, wakati wa mkutano kuelimisha watumishi kuhusu muswada huo, uliofanyika Januari 24, 2023 NIMR makao makuu, jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...