Na Karama Kenyunko Michuzi TV
WAZIRI Mkuu nchini Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ghafla ya utoaji wa Tuzo za Umahiri katika fasihi ya kiswahili zinazotolewa na Kampuni ya Vifaa vya Ujenzi ya ALAF.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Januari 19 2023 Meneja wa Uhusiano wa Kampuni hiyo Hawa Bayuni amesema kuwa Tuzo hizo zitatolewa Januari 25 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zilizopewa jina la Kiswahili Prize Award zinafanyika kwa miaka saba tangu zilipoanzishwa mwaka 2014 .

Bayuni amesema lengo la Tuzo hizo ni kuikuza lugha ya Kiswahili ambapo washiriki kutoka nchi mbalimbali zaAfrika ikiwemo Tanzania zitashiriki.

Amesema kuwa Tuzo hizo huchagiza kasi ya usambaji wa Kiswahili Afrika ikiwa sehemu ya kuzikamilisha ndoto ya kuiunganisha Afrika kwa lugha moja.

Katika Tuzo hizo zilizoasisiwa na Dkt.Lizzy Attree na Mukoma Ngugi Mshindi atapewa kiasi cha Dola za Kimarekani 5,000.
Meneja uhusiano wa ALAF, Hawa Bayuni akizungumza na waandishi wa habari juu ya Maandalizi ya Tuzo za Kiswahili Prize zitakazofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. kushoto ni Afisa uhusiano wa kampuni hiy Theresia Mwasy.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...