*Pata dhamana ya hadi 80% kutoka PASS Trust

TAASISI ya PASS Trust inayotoa huduma ya dhamana kwa wakulima wa kilimo biashara imesisitiza hayo katika warsha ya wadau wa kilimo biashara iliyofanyika kanda ya Magharibi Mkoani Tabora.

 Wakulima wamehaswa kutumia njia mbali mbali za kisasa katika uzalishaji kwa kuzingatia kanuni za ukuaji wa kijani shirikishi ambazo zinachochea utunzaji wa mazingira kwa kilimo endelevu.

Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa PASS Trust, Adam Kamanda, ameelezea fursa zilizopo PASS kwa wadau wa kilimo biashara katika kuwekeza kwenye miradi inayozingatia utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ambapo taasisi hiyo inatoa dhamana ya hadi 80% kwenye mnyororo wa thaman katika sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda na mazao ya misitu. 

Miradi hiyo ni pamoja na inayowekeza kwenye; matumizi bora ya maji, matumizi ya nishati mbadala, matumizi bora ya ardhi, inayozingatia urejeleshaji wa taka zitokanazo na shughuli za kilimo, matumizi ya mbolea asilia na miradi yote inayozingatia kanuni na taratibu zote za uhifadhi wa mazingira.

Lengo kuu la PASS Trust ni kuhakikisha wadau wa kilimo biashara wanaongeza tija katika shughuli zao huku wakitumia rasilimali vizuri, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kuleta uendelevu wa shughuli hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...